kwamamaza 7

Uganda yadaiwa kupeleka wanajeshi kimya kimya kwenye mpaka na Rwanda

0

Uganda inadaiwa kuwasambaza wanajeshi wake bingwa karibu na mpaka na Rwanda.

Rwanda pia mwezi uliopita ilidaiwa kuwapeleka wanajeshi wengi karibu na mpaka na Uganda.

Kwa mujibu wa chombo cha habari Elayama News, jambo hili ni baada ya kuongeza uwezo wa divijeni ya pili ya UPDF inayongozwa na Brig. Kayanja Muahanga Wilayani Mbarara.

Divijeni hii inaundwa na brigedi mbili; 309 na 401 ambazo zilipatiwa uwezo wa kutosha tangu mwaka 2018.

Mfano unaotolewa kuhakikisha hayo ni kuipeleka bataliyani ya 19 chini ya Kamanda Kanuni Emmanuel Mukasa katika maeneo ya Cyonyo, Rushaki,  Kamuganguzi, Butobere na Gafunzo. Maeneo yote yangali karibu na Rwanda.

Bataliyani nyingine zikiwemo ya 35 chini ya Kamanda Luteni Kanuni Johnson Muhanguzi, ya 33 chini ya Kamanda Luteni Kanuni Tumwine. Pia kuna brigedi nyingine chini ya Kamanda Kanuni Keith Katungyi inayoundwa na bataliyani mbili; ya saba chini ya Kamanda Meja  Geoffrey Nabimanya na ya 47 chini ya Kamanda Meja Jotham Kature.

Taarifa hizi zimeenea wakati ambapo kuna kutoelewana kati ya Rwanda na Uganda tangu miaka miwili iliyopita.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.