kwamamaza 7

Uganda: Wanyarwanda wawili wakamatwa kwa mashtaka ya mauaji

0

Polisi wilayani Kisoro imewakamata Wanyarwanda wawili kwa majina ya  Enock Mushengezi, 30, na Dusengimana Fotunatusi  , 32, wanaotuhumiwa  kumuua mwanamume  Samuel Safari,42 ,mkazi wa kijiji cha  Nyabiyonga  ijumaa wiki iliyopita.

Polisi imesema kuwa malehemu alipigwa chuma  kichwani na kuuawa hapo hapo.

Msemaji wa Polisi kwa eneo la Kigezi,Elly Maate  ametangazia Chimpreports chanzo cha  tukio hili kitajulikana baada ya polisi kufanya upelelezi wake.

Maate ameendelea wanakusanya vithibitisho husika ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani juu ya haya mashtaka.

Kiongozi wa ngazi za  chini,Hadard Nkunzimana amejuta hili kwa kusema kuna suala la usalama hasa usiku kutokana na ulevi.

Kuna taarifa kwamba watuhumiwa ni wazaliwa wa wilaya ya Gakenke,kaskazini mwa Rwanda.

Kwa kawaida Dusengimana Fotunatusi na Enock Mushengezi ni watmishi mjini Kisoro,Uganda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.