kwamamaza 7

Uganda: Wanyarwanda wawili wakamatwa kwa kumiliki bunduki na upelelezi kwa Rwanda

0

Wanyarwanda wawili kwa majina ya  Emmanuel Rwamucyo Rwamukinuzi na  Emmanuel Rwamucwe wamekamatwa wilayani Mbarara nchini Uganda kwa kumiliki bunduki kinyume na sheria na kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa za Chimpreports hawa walikamawa tarehe 26 Meyi  mwaka huu wakiwa na bunduki.

Hata hivyo, wanafamilia wa Rwamukinuzi wamesema madai ya kumiliki bunduki ni uongo mtupu.

“ Huu ni uongo mkubwa, hajui kwa nini wanamshtaki kumiliki bunduki” ndugu ye wa kike ameelezea Chimpreports

Hawa wamesema Rwamukinuzi alikuwa anataka kuhifadhi fedha zake UGX miliyoni 40 kwenye benki mjini Mbarara na kumuita rafiki yake Rwamucwe kabla ya kukamatwa.

Kwa sasa, hawa  wanafungwa gerezani Luzira mjini Kampala.

Ushirikiano kati ya Rwanda ulianza kuwa ovyo mwaka 2017 ambapo Wanyarwanda wengi walikamatwa na kuteswa kimwili na maafisa wa upelelezi wa  jeshi la Uganda (CMI) kwa mashtaka ya kuwa wapelelezi.

Rwanda ililaumu hivi vitendo kwa kusema hawa ni raia wanaokuwa nchini Uganda kwa shughuli zao za kawaida.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.