kwamamaza 7

Uganda: Wanyarwanda washtaki serikali kuwazuia kutembelea famila zao nchini Rwanda

0

Wanyarwanda wanaoishi nchini Uganda wanadai kuwa serikali inatia vizuwizi kutembelea familia zao nchini Rwanda.

Suala hili limezungumziwa wakati wa kusherekea  kuonja mazao maarufu kama ‘Umuganura’ wilayani Nakaseke nchini Uganda.

Mmoja wao, Joyce Kamukama ameeleza afisa kwenye mpaka wanagoma kuwarudishia vitambulisho vyao wanapoelekea nchini Rwanda.

Balozi wa Rwanda nchini Uganda, Rtd Meja Jen. Frank Mugambage ameeleza suala hili lipo na marais wa hizi nchi waliwahi kulijadili.

“ Mala nyingi tunazungumza na viongozi wa Uganda, ndio wanaotoa vitambulisho lakini kuna wakati ambapo wanawanyima Wanyarwanda hivi vitambulisho” amesema Mugambage

“Rais Kagame alizungumza na mwenzake kuhusu hili suala alipokuja huku siku zilizopita, walikubaliana kuwa litasuluhishwa” ameongeza balozi Mugambage

Hawa Wanyarwanda wameeleza hawana maelezo yoyote kwa nini haki zao zinakiukiwa kinyume na kuwa raia wa Uganda hawakabiliani na suala lolote kwenye mipaka na Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.