kwamamaza 7

Uganda: Wakazi wamshambulia mwanajeshi kwa kushirikiana na jambazi asili ya Rwanda

0

Wakazi wa eneo la Abaita, Entebbe, mjini Kampala wameshambulia mwanajeshi wa Uganda kwa majina ya Pvt Edgar Nalwasa kwa kusema anaunga mkono mwizi asili ya Rwanda.

Wakazi wameelezea Dailymonitor huyu mwizi alimnyanganya mwanamke kifurushi cha mikononi na walipoanza kumkimbiza akampigia simu mtu ili kumnusuru.

Shahidi wa hili tukio wameeleza wameshangaa kuona namna ambavyo humwanajeshi Nalwasa amejitokeza kwa ghafla. Kwa hiyo, wakaanza kudhani kuwa anashirikiana na huyu mwizi.

Mkazi ambaye hakutaka jina lake litiwe hadharani amehakikisha mwizi alikuwa Mnyarwanda.

Kwa sasa, huyu Mnyarwanda anatibiwa hospitalini Entebbe na mwanajeshi Nalwasa kuokolewa na jeshi la polisi.

Mkuu wa Polisi eneo la Entebbe, DPC Mission Samuel amesema hili limetokea lakini hakueleza  kwa mapana na marefu.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.