kwamamaza 7

Uganda: Tumaini za kumuona mkazi asili ya Rwanda aliyetekwa nyara ni kujikaza kisabuni

0

Tumaini za kumuona mkazi asili ya Rwanda Johnson Nuunu,60, aliyetekwa nyara tarehe 19 Disemba 2017 usiku  akiwa baani eneo la Rubaare,wilaya ya Ntungamo zimefifia  baada ya mafisa wa polisi kwenye kituo cha polisi cha Mbarara kuwambia wanafamilia yake kuwa jitihada zao ni bure,haziwezi kuwasaidia lolote.

Wanafamilia wa muathiriwa  wakiwemo bin yake Julius Kansiime,30, na mwenzake maarufu kama Katudu wametangazia Chimpreports kuwa walienda punde si punde kuwasilisha suala hili kwenye kituo cha polisi cha Rubaare lakini afisa wa polisi aliyekuwa na nia ya kuwasaidia alikataa na kuwacha ofisini akaenda zake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia, Kansiime amesema kuwa waliporudi kwenye kituo cha polisi siku nyingine  ilikuwa kama ni mala ya kwanza polisi kusikia suala hili ila OC CID ambaye amepigia simu mtu mwingine ambaye hakutambulika aliambiwa kuwa wanayemtafuta yupo bali wasipoteze muda,waende.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,Kansiime ameleza kuwa amejaribu kumuuliza afisa wa ndani ambaye hakutaja majina yake na kumuambia kuwa baba yake hayupo mjini Kampala,taarifa ambazo zimehakikishwa na binamu wake baada ya kupigia simu kituo cha polisi mjini Mbarara na kujibiwa kuwa hayupo.

Johnson Nuunu ni tajiri mkazi wa kijiji cha Rukiri,kata ya Kayonza,wilaya ya Ntungamo.Kuna taarifa kwamba mala nyingine anatembelea mjini Kigali na kuwa bintize wawili waliolewa nchini Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

  

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.