kwamamaza 7

Uganda:  Mwalimu asili ya Rwanda akamatwa

0

Mwalimu asili ya Rwanda, Daniel Karangwa amekamatwa Wilayani Kiboga nchini Uganda kwa sababu ambazo hazijatangazwa.

Karangwa,46, alikamatwa tarehe 24 Machi 2019, alipokuwa shuleni Rwamata Summit College kama alivyoeleza mwanafamilia wake.

Kwa mujibu wa Chimpreports, ofisa wa jeshi alimuambia kwamba anatakiwa kwenye kituo cha polisi cha Rwamata alikofungiwa kabla ya kupelekwa mjini Kampala.

“ Polisi hawajatuambia kwa nini amekamatwa.” Amesema Fred, mmoja mwa wanafamilia wake.

“Tunaomba serikali kutujulisha alipofungiwa Karangwa ili tuweze kuwasiliana naye.” ameongeza

Karangwa amekamatwa wakati ambapo maafisa wa upelelezi nchini humo wanakusanya Wanyarwanda juu ya kutuhumiwa kuwa wapelelezi.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.