kwamamaza 7

Uganda: Mnyarwanda ashtakiwa kuwaua watu na kuwapokonya ardhi yao

0

Mnyarwanda kwa majina ya Isaac Ndahiro anashtakiwa kuwaua raia Wilayani Kiruhura nhini Uganda katika fujo la kuwapokonya  ardhi yao.

Mmoja mwa waliopokonywa ardhi, bikizee Hariet amesema fujo hili limemfanya kumaliza miaka 18 bila ardhi.

“ Angalia ngozi yangu, miguu yangu ilivimba,ninaishi katika hali mbaya” Hariet ametangazia NTV kwa kutumia Lunyankole.

Wakazi wa huko wamehakikisha ardhi hii ni ya mume wa Hariet, malehemu Christopher Kajundira ambaye alihama huko tangu mwaka 1965.

liipokonya familia yake Isaac Ndahiro ambaye ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa (YUNA).

“Ardhi hii ni yam zee Kajundira,alikuja na watu wake wakaishi huku miaka kadhaa iliyopita” ameleleza Mkurugenzi wa Tume  ya masuala ya ardhi nchini,  Catherine Bamugemereire.

Kuna taarifa kwamba fujo la kupokonya ardhi la  mwezi  Novemba 2017, Ndahiro aliwaua watu alivyokuwaakihojiwa na Tume ya masuala ya ardhi.

Ndahiro alikubali kuwa kuna mwanamke mjamzito aliyeuawa pamoja na kuwajeruhi wanawe wa kike na wa kiume.

“Je, huo ni mtindo wa haki gani? Unaweza kufanya hayo nchini Rwanda” Catherine amemuuliza Ndahiro

Kwa hayo, Mkurugenzi wa Tume  ya masuala ya ardhi nchini,  Catherine Bamugemereire amewaonya polisi, Ndahiro na wafanyakazi wake kukoma vitendo vya kuwaonea wakazi.

“Nitakaposikia kwamba amewashambulia tena wale wanawake nitakuja kwa kichwa chako” ameonya bugemereire kwa kumnyoshea kidole Ndahiro.

Kwa sasa, Ndahiro anafanyia  shughuli zake za kufuga wanyama kwenye hii ardhi.

Kuna taarifa kwamba huyu Ndahiro anamiliki ardhi ha 562 nyingine Wilayani Mbarara.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.