kwamamaza 7

Uganda: Kesi ya Mnyarwanda anayetuhumiwa kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame yahairishwa

0

Kesi ya Mnyarwanda Rene Rutagungira ambaye anatuhumiwa kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame Luteni Joel Mutabazi yahairishwa baada ya wanasheria kwenye kesi hii kukosekana mahakamani  Makindye, mjini Kampala.

Chimpreports imeeleza wanasheria Caleb Alaka Evans Ochieng na  Frank Kanduho hawakuelezea mahakama sababu ya kutoonekana mahakamani.

Kwa hili, mwendeshamashtaka wa serikali, Meja Raphael Mugisha ameelezea mahakama hatatangaza lolote kuhusu upelelezi waliofanya khusu kesi hii.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa koti ya jeshi ya Makindye, Luteni Jenerali Andrew Gutti amewaambia washtakiwa kuwajulisha wanasheria wao kwamba kesi itaendelea tarehe 26 Juni 2018.

Rene Rutagungira na wenzake saba wakiwemo maafisa wakuu wa polisi nchini Uganda wanashtakiwa kumiliki mabomu na kuwateka nyara Wanyarwanda na wakiwemo aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame Luteni Joel Mutabazi na mwenzake Jackson Karemera terehe 25 Otctoba 2013 wilayani Mpigi eneo la Kammengo.

Ikumbukwe kwamba Luteni Joel Mutabazi alihukumiwa mwaka 2014 kufungwa maisha jela juu ya uhalifu wa kuungana mkono na wanamgambo wa FDLR na RNC ya Jenerali Kayumba Nyamwasa.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.