kwamamaza 7

Uganda: Jen. Kale Kayihura akamatwa

0

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi ya Uganda, Jen. Kale Kayihura  pamoja na wenzake  ambao idadi yao yaijajulikana wamekamatwa na jeshi la Uganda.

Kwa mjibu wa Dailymonitor, Kayihura amekamatwa akiwa nyumbani kwake kijijini Kashagama wilayan Lyantonde saa chache zilizopita.

Hiki chombo cha habari kimeeleza Jen.Kayihura amepelekwa mjini Kampala ili kuhojiwa kuhusu masuala ambayo hayajatambulika.

Hili ni baada ya wanajeshi jumanne kuja kumtafuta nyumbani kwake na kumkosa.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Brig. Richard Karemire amehakikisha hizi taarifa.

“ Jana  wanajeshi walikuenda kumkamata ili aeleze Mkuu wa jeshi la UPDF, Jen. David Muhoozi  lakini alikuwa hayupo nyumbani,alikuwa  Mbarara. Leo ndege imerudi kwake kumleta  kwenye kituo cha jeshi Mbuya”

Pamoja na hayo, haijaeleweka waziwazi kwamba Kayihura amefungwa jela

Kayihura alifukuzwa kazini na Rais  Museveni tarehe 4 Aprili 2018.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.