kwamamaza 7

Uganda inaongoza kwa kuzungumza kingereza barani Afrika

0

Uganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya Kingereza kwa ufasaha barani Afrika. Utafiti uliofanywa na shirika la lugha duniani World Linguistic Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika Kusini ikiwa katika nafasi ya tatu na Kenya katika nafasi nne

Kulingana na gazeti la The New Vison nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya video iliomuonyesha malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea kiingereza.

Rwanda iliokuwa chini ya koloni ya Ufaransa ilianza kuzungumza Kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa. Rwanda baada ya hapo iliingia katika jamii ya nchi ambazo hutumia lugha ya kingereza “Commonwealth” mwaka wa 2009.

Gazeti la The New Vision linasema kuwa kiingereza nchini Uganda ndio lugha rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini humo.

Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi.

The New Vison linasema kuwa hivi majuzi serikali iliziagiza shule kufunza lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini ikasisitizia kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala.

Mataifa yanayozungumza kiingereza kwa ufasaha:

1.Uganda

2. Zambia

3. South Africa

4 . Kenya

5. Zimbabwe

6. Malawi

7. Ghana

8. Botswana

9. Sudan

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.