kwamamaza 7

Uganda: Chombo cha habari chadaiwa kuungana mkono na chama cha Jenerali Kayumba Nyamwasa

0

Chombo cha habari The New Vision kimedaiwa kuungana mkono na Chama cha Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa, Rwanda National Congress (RNC ) kupitia Ofisi ya upelelezi wa jeshi nchini Uganda (CMI).

Taarifa za chombo cha habari Virunga Post ni kwamba  The New Vision inashirikiana na CMI kuficha  hadhira ukweli kuhusu vitendo vya kusajili wanajeshi wa RNC na visa vya kuwakamata na kuwatesa Wanyarwanda kwa kuwashtaki kuwa wapelelezi wa Rwanda nchini Uganda.

Kiongozi wa CMI, Bri.Jen. Abel Kandiho/picha na intaneti

Virunga Post iliandika” Habari ilioyandikwa na The New Vision” Why Museveni Sacked Senior Imigration officials?… The New Vision ilitangaza ni kutokana na kuwa waliokuwa wakiwakamata wakimbizi asili ya Rwanda walikuwa na vitambulisho vya Uganda.Haya ni maneno yanayostahili kuwa na uthibitisho.CMI wala The New Vision hawana wowote,hakuna”

“ Haya mashtaka ya kuwakamata Wanyarwanda yalikuwa yanalenga kuifanya hadhira kusahau ushirikiano ulioko kati ya CMI na RNC” Virunga Post iliongeza

Mwenyekiti na Kiongozi wa Chama cha RNC, Jen.Kayumba Faustin Nyamwasa/Picha na Reuters

Hiki chombo cha habari  kilieleza  CMI inatumia The New Vision  kuwasilisha propaganda zake ili kuharibu ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda.

Pia, Virunga Post ilitangaza The New Vision kwa msingi wa propaganda ilitia upande ukweli kisha ikaamua kuandika uongo.

“Wanyarwanda waliotajwa katika ile stori,  walirudishwa nchini Rwanda kulingana na sheria,kuna mkataba kati ya Polisi ya  Rwanda na Uganda kuhusu hili suala. The New Vision ilijisahaurisha hili”

Pamoja na hayo, hiki chombo cha habari kilisikia mala kiliandika kikihakikisha kuwa bilashaka  kuna ushirikiano kati ya CMI na RNC.

Kiliandika” Mwezi Disemba, Wanyarwanda 43 waliokamatwa kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania(kikagati) walikuwa wakielekea  eneo la Minembwe,nchini DR Congo kwenye kambi za jeshi la Kayumba Nyamwasa kwa msaada wa CMI”

Hata hivyo,RNC kupitia msemaji wake Jean Paul Turayishimiye kwenye mazungumzo na sauti ya Marekani, alikanusha haya mashtaka kwa kusema chama chao hakina kambi za jeshi nchini DR Congo.

Virunga Post ilijulikana mno  mwaka jana ambapo ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda ulianza kuwa ovyo kutokana na upelelezi,kuwateka nyara wakimbizi,kuwakamata na kuwatesa Wanyarwanda nchini Uganda na mengine.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.