kwamamaza 7

Uganda: Afisa kwenye ikulu adaiwa kuipaka masizi Rwanda

0

Afisa kwa wajibu wa mawasiliano ya Rais Museveni, Sarah Kagingo anadaiwa na vyombo vya habari nchini Rwanda kuwa anapaka masizi serikali ya Rwanda.

Chombo cha habari Igihe kimetangaza  Kagingo anapitisha propaganda dhidi ya Rwanda kupitia Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi nchini Uganda (CMI).

Kwa mujibu wa hizi taarifa, Kagingo anaandika hizi propaganda kwa kutumia majina yasiyo yake maarufu kama Goreth Ofungi kwenye chombo cha habari anachomiliki kwa jina la Softpower.

Mala nyingi vyombo vya habari nchini Uganda kama Chimpreports na Softpower vilinyoshewa vidole kulenga pia kuipaka masizi serikali ya Rwanda.

Hizi taarifa zilienea tangu mwaka jana, Kwa sasa, pande zote mbili yaani Rwanda na Uganda walikuwa wakisema kila upande unatumia vyombo vya habari kurushia matope upande mwingine.

Kwa hili, Uganda ilisema Rwanda inatumia mitandao ya kijamii hasa Tiwtter na vyombo vya habari nchini Kenya  kama vile Daily Nation na Stardmedia kupasha propaganda zinazoipaka masizi.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.