kwamamaza 7

Ufaransa:Mtafiti aeleza kwa nini Ufaransa haiwezi kukubali kuwa EX-FAR walidungua ndege iliyokuwemo Rais Juvenal Habyarimana

0

Mtafiti na muandishi,asili ya Ufaransa Jacques Morel kwa ubingwa wake wa miaka ya 12 ya utafiti kuhusu ushiriki wa Ufaransa nchini Rwanda,ameleza kuwa Ufaransa haiwezi kukubali kuwa ndege aliyokuwemo Rais Habyarimana ilidungulia na EX-FAR.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Jacques Morel kupitia kitabu chake kwa jina’La France au Coeur du Genocide’yaani Ufaransa katika moyo wa mauaji ya kimbali,anasema kuwa Ufaransa unafanya hili kwa kuwa ikikubali itamaanisha kuwa walishirikiana na waliomuua Habyarimana kwa kuwa walikuwa wakisadia mno jeshi la EX-FAR.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya Ufaransa kuanzisha upelelezi kwa mala ya tisa kwa kujua walioidungua Ndege ya Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994.Kisa hiki kilizusha utata kwa kuwa upande mmoja wa watafiti walionyesha kuwa ndege hii ilidunguliwa  kwa ushiriki wa Ufaransa na upande mwingine kueleza kuwa RPF ndio walioidungua.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akizungumza na Sputnik France,Jacques Morel ameleza kuwa wabunge wa ufalansa ndio walioanzisha haya mambo ya upelelezi mnamo mwaka 1998.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Suala la ushirikiano mbaya kati ya Ufaransa na Rwanda mala nyingine husababishwa na kukanusha kwa Ufaransa kuhusu mchango wake katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.