kwamamaza 7

Ufaransa:Mnyarwanda afutwa kazi juu ya mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbali

0

Hospitali ya serikali kwa jina la Paul Doumer, nchini Ufaransa imefukuza kazini daktari,asili ya Rwanda,Dk.Charles Twagira anayeshtakiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 nchini Rwanda.

Hili ni baada ya Tume ya kupambana na mauaji ya kimbali nchini Rwanda juma tatu kupiga marufuku kuajiriwa kwake Dk.Charles Twagira mwezi uliopita.

Tume hii iliweka wazi kwamba kuajiriwa kwake ni kama vile kuidhihaki mauaji ya kimbali nchini dhidi ya Tutsi  mwaka 1994.

Hospitali Paul Doumer imetangazia The Associated Press kwamba ilijuwa haya mashtaka wiki moja tu  baada ya Dk.Charles Twagira kuajiriwa.

Hospitali imeongeza kwamba imeamua hili  baada ya uhakikisho wa mwendeshamashtaka wa mji wa Paris na kuwa uamuzi huu utasaidia kutoa huduma nzuri kwa jamii.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mshtakiwa anakanusha mashtaka yote kupitia mwanasheria wake,Arthur Vercken kwamba mashtaka haya ni msukumo wa kisiasa wa serikali ya Rwanda na kuwa hospitali ilijulishwa kuhusu haya mashtaka kabla ya mteja wake kuajiriwa.

Dk. Charles Twagira alihukumiwa  kufungwa maisha jela bila kuwepo mwaka 2009 juu ya kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.