Swahili
HABARI MPYA KIMATAIFA SIASA

Ufaransa:Francois Graner kushtaki tena halmashauri ya kulinda katiba

Mtafiti, Francois Graner ametangaza kwamba anajianda vilivyo kushtaki halmashauri ya kulinda katiba nchini Ufaransa kwenye mahakama ya ulaya ya kulinda haki za binadamu(CHED) baada ya kukataliwa upatikanaji wa hati zenye vitendo vya Mitterand nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Mtafiti,Francois Graner

Kupitia mazungumzo na Jeune Afrique,Graner amesema kuwa uamuzi uliotolea  na halmashauri ya kulinda katiba ulikuwa wa kisiasa pia mbaya kulingana na haki za binadamu na kuwa ulimuudhi.

Me Spinosi nami tunajianda kufanya jambo hili”amesema Graner.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Francois Graner ameongeza kwamba anaamini mahakama ya Ulaya kwani ina uwezo na kuwa mala nyingine inalinda haki za binadamu na mikataba yake husika barani ulaya.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,Graner amesisitiza kwamba mkurugenzi wa halmashauri  ya kulinda katiba,Laurent Fabius na mwenzake Lionel Jospin waliowahi kuwa mawaziri wakuu kwenye serikali ya Rais Mitteranda waliamua kisiasa tatizo linalowahusu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya mahakama kuu nchini Ufaransa kuhukumu kwamba mtafiti,Francois Granner hana rukhusa ya upatikanaji wa hati zenye vitendo vya Mitterand nchini Rwanda na kuwa hati hizi zitatiwa hadharani mwaka 2021.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com