Home HABARI MPYA Ufaransa ulikiuka sheria za kimataifa zinazohusu mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi- Madai kwa UN
HABARI MPYA - SIASA - July 1, 2017

Ufaransa ulikiuka sheria za kimataifa zinazohusu mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi- Madai kwa UN

Shirikisho la mashirika ya kuwatafuta na kuwapeleka mahakama wahalifu wa mauaji ya Kimbari dhidi ya watutsi wanaoishi Ufaransa (CPCR) limepeleka madai yao kwa Idara ya Haki za Kibinadamu Alhamisi tarehe 29 Juni la Umoja wa Mataifa ikieleza wasiwasi wao kwamba Ufaransa ulikiuka sheria za kimataifa kuhusu Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994.

Ibuka ambayo ni Shirika linalotetea haki za manusura wa Mauaji ya Kimbari iliunga mkono hatua hii na kuihimiza idara ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na Hata nchi wanachama wa UN kuyatilia maanani madai haya ya (CPCR) yaliyoasilishwa kwa idara ya Haki za Kibinadamu kuhusu ya ukiukaji wa sheria za kimataifa zinazohusu Mauaji ya Kimbari dhidi ya watutsi ya 1994.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Dkt. Jean Pierre Dusingizemungu amesema “ tunawatolea wito Idara ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na hata nchi nyingine wanachama kuutangaza hadharani uhusikaji wa Ufaransa katika mauaji ya Kimbari dhidi ya watutsi na hata kuchukua hatua kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa”

“Tungependa hata kuwaomba Ufaransa kuwapeleka nchini Rwanda ama kuendesha kesi za Wanyarwanda ambao wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi wanaoendelea kuhifadhiwa na Ufaransa” ameongeza

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ibuka iliwaomba pia Ufaransa kuweka hadharani taarifa zote zinazohusu Mauaji ya Kimbari, kuheshimu sheria za kimataifa kwa kuwapeleka Rwanda wanyarwanda wanaotuhumiwa uhusikaji katika mauaji ya kimbari dhidi ya watusi, kuheshimu pia sheria za kimataifa kwa kuendesha kesi za wanyarwanda wanaotuhumiwa uhusikaji katika mauaji ya kimbari wanaoishi Ufaransa na hata kushirikiana na nchi ya Rwanda kwa kuwatolea haki manusura wa mauaji ya kimbari ili kuhamasisha safari yao ya umoja na maridhiano.

Madai haya yanazuka ikiwa Ufaransa unatarajia kupokea mkutano wa Uzinduzi wa Ukaguzi wa Haki za Binadamu wa kimuda (Universal Periodic Review) wa kuchunguza jinsi nchi wanashirika 194 zinavyoheshimu Haki za Kibinadamu. Lengo kuu ya Ukaguzi huu ni kuboresha hadhi ya haki za kibinadamu kwa ajili ya mabadiliko ya wakazi wa dunia.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.