kwamamaza 7

Uchaguzi waanza rasmi kwa wanyarwanda wa Diaspora- Waziri Mushikiwabo awatakia uchaguzi mwema.

0

Ikiwa siku ya leo tarehe 3 Agosti ni siku ya Uchaguzi wa rais atakayeiongoza Rwanda kwa kipindi cha miaka 7 itakayokuja, wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi yaani(Diaspora ) wamekwisha anza uchaguzi.

Wanyarwanda waliotangulia wengine ni wale wanaoishi nchi za Azia hasa hasa Ujapani na Uchina ambako kuna wanyarwanda wengi wanaokaa nchi hizo.

Waziri wa mambo ya nje ya nchi Bi Mushikiwabo Louise amachapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwatakiya wanyarwanda hao kuwa na uchaguzi mwema. Na kusema  kwamba ndio kichamsha kinywa

 

Bangalore

Katika mji huu wa India napo uchaguzi umekwisha anza ambapo wanyarwanda wapatao 100 wanatarajiwa kupiga kura. Mji huu unakaliwa na wanyarwanda hususani wanafunzi wanaofuata masomo yao. Rwibasira Mike ambaye ni mkuu wa wanafunzi wanaofuatia kisomo chao India amiambia Bwiza.com kwamba wanyarwanda wa hapo wanashiriki uchaguzi kwa wingi na wana msisimko wa kiasi fulani.

Ubelgiji

Wanyarwanda wanaoishi Ubelgiji nao wameanza uchaguzi rasmi ambapo shughuli zake zinaongozwa na Balozi wa Rwanda nchi humo Nduhungirehe Olivier ambaye ameanza kwa kuonyesha visanduku vya kura vikiwa wazi kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo.

Balozi Nduhungirehe

Etiopia

Wanyarwanda wanaoishi nchini Etiopia nao hawakukosa kushiriki shughuli hii ya uchaguzi inayoashiria uzalendo.

Balozi Hope Tumukunde akila kiapo kabla kura ya kuanza

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.