Wagombea wa chama cha upinzani nchini Rwanda, Democratic Green Party of Rwanda (DGPR) wametangaza watakapochaguliwa watapunguza kodi kwa biashara ndogo.

DGPR wametangazia wakazi wilayani Kirehe, mashariki mwa Rwanda kuwa kuna mengi yaliyotekelezwa na mengine ambayo hayajakamilishwa bado.

Mmoja mwa wagombea wa hiki chama, Jean Marie Vianney Mwiseneza amesema” Hatutarudisha nyuma mema ambayo serikali ilitimiza lakini mabaya yataondolewa tutakapocaguliwa kuwa bungeni. Kuna mambo kama maendeleo ya vijana, kuondoa kodi za ardhi”

Mmoja  mwa wakazi Wilayani Kirehe ameambia Bwiza.com wanataka DGPR kutimiza mipango yao yote watakapochaguliwa.

“ Wana miradhi mizuri. Jambo la kupunguza kodi ni suala kubwa, unaombwa kodi kila mala unapoenda sokoni, mambo ya bima ya afya na mengine”

Kiongozi wa DGPR, Dk. Frank Habineza  amesisitiza watatimiza waliyoahidi hasa suala la kuongeza nguvu za usalama.

Chama cha DGPR kinawakilshwa na wagombea  wa ubunge 32 ambao watawania ubunge tarehe 2 mwezi Septemba 2018.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.