Home SIASA Uchaguzi wa Rwanda ulikidhi vigezo vya kimataifa- Waangalizi wasema.
SIASA - August 7, 2017

Uchaguzi wa Rwanda ulikidhi vigezo vya kimataifa- Waangalizi wasema.

Waangalizi wa uchaguzi waliotumwa kutoka mashirika na vyombo mbalimbali hususani vya Afrika wasema uchaguzi ulikwenda vizuri hadi kukidhi viwango vya kimataifa.

Waangalizi ambao walishiriki uchaguzi wa Rwanda ni kutoka Umoja wa Afrika(AU), Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC), Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki na Kusini ( COMESA) na Kongamano la Kimataifa la Eneo la Maziwa Makuu(ICGLR).

Wajumbe kutoka mashirika hayo yote walisema uchaguzi umekuwa huru na wazi

Kabla ya Waangalizi hawa wote kutumwa nchini kote  walifanya mikutano na wadau wote wa shughuli hii wakiwemo mojawapo ya wagombea, Tume ya Uchaguzi, Polisi, Mashirika ya Kijamii, na wengineo.

Rais wa zamani wa Mali, Dioncounda Traore ambaye amekuwa kiongozi wa waangalizi kutoka ujumbe wa AU ambao walitumwa wilaya 30 nchini kote, alisema hakuwa na ukiukaji wowote wa kisheria katika zoezi hili. Alisema pia kuwa kulingana na taarifa walizopewa na wadau mbalimbali wa shughuli hii ni kwamba waliridhika na zoezi hii.

Jambo jingine ambalo walilisifu kama umaalum wa Uchaguzi wa Rwanda ni kutotumia fedha nyingi ambapo alisema nchi nyingine za Afrika huwa zinatumia bajeti kubwa kwa zoezi la uchaguzi wakati ambapo Tume ya Uchaguzi ya Rwanda iliamua kuwatuma wafanyakazi wa kujitolea. Matunda ya mfumo huu yalikuwa kupunguza bajeti ya awali kwa zaidi ya nusu.

Wajumbe hawa walisifu zoezi nzima la uchaguzi na jinsi wananchi walivyoishiriki na hasa mfumo wa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa kuaminiwa.

Walisifu pia tabia za wagombea katika uchaguzi huu ambao walikubali matokeo ya uchaguzi bila kuzua mizozo yoyote kama inavyotokea kwa nchi nyingi za Afrika.

Wajumbe hawa pia hawakukosa kugusia uwazi uliokuweko katika zoezi hili kwa kuwaacha wagombea na muda sawa na hata kwa vyombo vya habari hususani vya kitaifa.

Jambo ambalo lilifanywa la kuwahimiza wagombea kuwatuma wasimamizi wao kwenye vituo vya uchaguzi vya nchi yote lilisifiwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hapa Frank Habineza alisema aliwatuma wasimamizi wapatao 500 na Mpayimana 100. Chama cha RPF ndicho kilichoweza kuwatuma waangalizi wake kwenye vituo vyote vya Uchaguzi.

Kulingana na matokeo ya Uchaguzi wa Rwanda ya muda , Paul Kagame aliushinda kwa asilimia 98.4 kama Tume ya Uchaguzi ilivyoeleza.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa mnamo siku za karibu kulingana na kanuni za uchaguzi ambapo matokeo yanapaswa kutangazwa mnamo siku saaba tangu uchaguzi kufanyika.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.