kwamamaza 7

Ubelgiji : Munyarwanda kauawa na mchumba wake

0

Kijana mwenye umri wa miaka 32 anaetambulika kwa jina la Benjamin J. anayeishi sehemu za Zeebruges nchini Ubelgiji yakamatwa akishtakiwa kumuua msichana kutoka Rwanda mwenye umri wa miaka 33 anayeitwa Ingabire Joselyne aliyekuwa mchumba wake. Inasemekana kuwa ilikuwa Ijumaa ya wiki jana alipompiga hadi alipovuja damu ndani ya ubongo na kusababisha kifo hicho.

Marafiki wa hawa wapenzi walipongeza mapenzi ya hawa wachumba, wakati walipotangaza uchumba wao, hapo mwezi Machi wa mwaka jana kupitia facebook, lakini baada ya mwaka mmoja tu amuua mchumba wake kwa kifo cha unyama ambacho kiliwahuzunisha sana wakazi wa jimbo la Wallon.

Kisa hiki kilitokea kwenye nyumba inayojulikana kama New Grand Park iliyoko karibu na barabara la Noorhinder mjini Zeebrugges ambamo walikuwa wakiishi pamoja kwa mjibu wa taarifa ya kw.knack.be

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hii inaendelea kusema kuwa mchumba wa Ingabire alimpiga hadi alipovuja damu ubongoni. Jirani wa hawa wariarifu kuwa wachumba hawa walikuwa wamelewa kwa pombe. Benjamin baada ya kumpiga mchumba wake aliita msaada ila amekuwa amechelewa kwa kuwa walifika wakati ambapo haingewezekana kutoa msaada wowote.

Baada ya kisa hiki polisi ilimkamata Benjamin J. na kumhoji, lakini idara ya uendeshaji mashtaka haikupenda kusema mengi zaidi ila tu wameshaanza upelelezi.

Kama ilivyoarifiwa na majirani zao, wachumba hawa wamekuwa wakiishi katika hali ya ugomvi wa kila siku na polisi imekuwa ikititokea mara nyingi kwa ajili ya mambo kama haya.

Jirani hawa walidai kuwa kelele za ugomvi wao zilikuwa zikiwasumbua na kuwafanya kutosinzia, walisema zaidi kuwa wangenshinda usiku wakigombana na asubuhi wakapatikana barabarani wakishikana kidole, ila kwa mara hii mambo yaligeuka huzuni tupu.

Wakati ambapo Benjamin yuko kizuizini kwenye kituo cha polisi kunasubiliwa maamzi ya kuwa ataachiliwa ama kesi yake itaendeshwa angali gerezani.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.