Home SIASA Twagiramungu alikuwemo mwa waliokuwa wakiniomba kuwa rais-Kagame
SIASA - July 30, 2017

Twagiramungu alikuwemo mwa waliokuwa wakiniomba kuwa rais-Kagame

Baada ya watu wengi kuonyesha hisia zao kuwa wanamwunga mkono rais Kagame ikiwemo wanavyama kutoka vyama nane vilivyojiunga na RPF na hata  wanasiasa wengine Kagame naye afichua kwamba muda tu baada ya kushinda vita vya ukombozi napo alipokea maombi ya watu wengi wakimtaka kutawala nchi kama rais na kwamba alikuwemo Twagiramungu Faustin.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Paul Kagame ambaye anawania kiti cha urais wa kuitawala Rwanda amesema haya akiwa kampeni mbele ya raia wa wilaya ya Nyamasheke alipokuwa akijibu maneno ya seneta Makuza Bernard aliyesema anamchukua Kagame kama mtu wa aina yake.

Seneta Makuza alisema kwamba wakati RPF iliposhika utawala wa Rwanda wanasiasa wengi walionyesha kwamba wanamtaka Kagame kuwa Rais  wa Rwanda.

Ingawa seneta Makuza hakuwataja wanasiasa hao Paul Kagame aliwaeleza kwamba miongoni mwa wanasiasa hao alikuwemo Twagiramungu Faustin ambaye kwa sasa yuko uhamishoni na ni mwenyekiti wa chama cha upinzani kisicho halali.

“mara baada ya vita vyo ukombozi kukamilika tuliiunda serekali ya umoja, na kumekuwa na watu wengi akiwemo Twagiramungu nadhani ndiye Makuza aliyemtaja ambaye yuko uhamishoni na ambaye tumemwomba mara nyingi kurudi kwenye nchi yake akatataa… alikuwepo, kilichonishangaza ni kwamba walikuja wakiwa kikundi cha watu wengi wakiwemo wanavyama PL,  wa PSD na wengine, Twagiramungu alikuwa mwenyekiti wa chama cha MDR. Tuliwaonyesha mpango wa jinsi mambo atafanyika na kilichonishangaza mno ni kwamba huo huo ambaye Makuza amekuwa akimtaja ndiye aliyeniambia kwamba ni mimi nayestahili kuwa rais”.

Hapa rais Kagame alisema kwamba baada ya muda si mlefu Twagiramungu alibadili mawazo kwamba hamtaki kamwe rais Kagame na kusema “huenda alidhani kuwa nitakuwa mtumishi wake ama daraja la kuvukia”

Paul Kagame ambaye kwa sasa yuko kampeni za kuwania urais wa Rwanda kwa muhula wa Tatu amepata uwezo huu baada ya katiba ya Rwanda kufanyiwa marekebisho kufuatia kura ya maoni iliyokuwepo baada ya wananchi kuasilisha nyaraka kwa bunge wakiomba marekebisho ya katiba.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.