kwamamaza 7

Tume ya Uchaguzi ya Rwanda inatarajia waangalizi wa Uchaguzi wengi

0

Tume ya Uchaguzi ya Rwanda imetangaza kwamba mpaka sasa imekwisha pokea maombi 100 ya waangalizi wa kura huku ikiwa na imani kuwa huenda idadi hii ikaongezeka mara 10 wiki zijazo.

Kwa mujibu wa habari alizoitangazia gazeti la The New Times la Rwanda ,Charles Munyaneza,katibu mtendaji wa Tume hii waangalizi hawa watafika kwa idadi kubwa.

“Tumekwisha toa idini kwa waangalizi 100 na wengine wanatarajiwa kuidinishwa wiki hii na kwa hivyo idadi yao itaongezeka sana katika siku zitakazokuja” Katibu Munyaneza asema

Katibu huu aliongeza kwamba miongoni mwa walioidinishwa ni mojawapo wa maafisa wanaofanya shughuli za kidiplimasia nchini, waangalizi wa uchaguzi kutoka Afrika ya Masharika na hata waangalizi wa nyumbani wa kujitegemea.

Vyama vya siasa na muungano wa shirika la jamii hawajawasilisha maombi yao ya uangalizi wa kura na kunasubiriwa pia waangalizi kutoka mashirika ya kimataifa na washirika mbalimbali wa maendeleo.

Vyama vya siasa vina hadi tarehe 15 kuasilisha orodha wa waangalizi wa uchaguzi wao, na tunaweza kusema tutakuwa na waangalizi zaidi ya 1000 kutokana na hali ilivyo sasa.

Kila chama cha siasa au mgombea binafsi anaruhusiwa na sheria kuwa na mwangalizi msimamizi wake katika kila kituo cha uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ingawa muungano wa shirika la jamii unatarajiwa kumpeleka mwangalizi wake katika kila tarafa kunasubiriwa, kwa mjibu wa Jean-Léonard Sekanyange, waangalizi 208 tu ambako kuna tarafa zifikazo 406 nchini kote. Ameongeza kwamba hawataweza kutuma waangilizi nchini kote kwa sababu ya kuwa na bajeti ndogo.

“Tumekwisha andaa orodha ya waangalizi wa kula 208 ambao hawatakuwa wakutosha kutumika katika tarafa zote 416 za nchi na ni kwa sababu ya kutokuwa na bajeti ya kutosha lakini tumejaribu kuwatafuta watakao tumika katika nusu ya tarafa zote”

Amendelea kuahidi kwamba zoezi la Kamati ya Uchaguzi ya Rwanda kuwatangaza wagombea halitakuwa na pingamizi yoyote na kuahidi kwamba uchaguzi wa Agosti mwaka huu utakuwa huru na tulivu.

“tunaendelea kuwahimiza vyombo vya habari kutoa nafasi na muda sawa kwa wagombea” ameongeza

Uchaguzi huu wa rais utafanyika tarehe 3 kwa Wanyarwanda wakazi wa diaspora na 4 ndani ya nchi mwezi Agosti ambako mpaka sasa tunasubiri wagombea rasmi kutangazwa baina ya wale sita ambao wamekwisha wasilisha nyaraka zao kwa tume ya Uchaguzi

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.