kwamamaza 7

Tume ya uchaguzi ya Rwanda iko tayari kwa udukuzi wa kura wa mtandao

0

Ikiwa suala hili la kuvamia na kudukua mifumo ya uchaguzi mtandaoni lilijitokeza sana kwenye nchi za kuheshimiwa kama Marekani katika uchaguzi uliofanyika siku za hivi karibuni na hata Ufaransa ambao kunakisiwa kuwa wadukuzi kutoka nchi za kigeni walioingia kwenye mifumo ya kura mtandaoni na kubadili mengi na kwa hivyo kufanya matokeo yake kuzua gumzo.

Kwa kutaka kujua mengi kuhusu jinsi Tume ya uchaguzi imejiandaa kujilinda na wadukuzi kama hawa Bwiza.com imeongea na Mike Shima Senga mwenyekiti wa taasisi ya Teknolojia na mawasiliano na kutuambia jinsi ambayo mfumo wa Tume hiyo uko salama

Akiuulizwa ikiwa kuna mbinu zozote za kupambana na udukuzi unaoweza kuzuka alisema

“tunajua kuwa swala hilo lilijitokeza kwenye nchi nyingi na kwa hivyo tulichukuwa mikakati ya kupambana nalo na naweza kusema kwamba tuko salama kwa asilimia 98 na 99.

Kikosi chetu cha wafanyakazi wa tekiniki wana ustadi wa juu wa kitekiniki na tuna mfumo wa kawaida wa kulinda  mifumo yetu ya habari.

Tuna matumizi maaum ya neno siri na vinginevyo.

Tumeweka pia kikosi cha wafanyakazi ambao wanajadili na usalama wa habari zetu za mtandao kwa kuchunguza ikiwa kuna wanaothubutu kuingia mifumo yetu na kwa hivyo tukichunguza hayo yote naweza kusema kwamba tunasimama vizuri.

Alipoulizwa ikiwa kuna kesi kama hizi zilizojitokeza alisema kwamba hawezi kusema eti mifumo yao iliweza kushambuliwa kwa sababu hakuna yeyote aliyeweza kudukua habari zao bali tu kuna wakati walipoona watu kutoka nchi za ng’ambo wakijaribu kuingia kwenye mifumo yao ya habari na wakashindwa kujua sababu yake.

Taasisi ya mawasiliano na teknolojia ya tume ya uchaguzi huwa ina kazi nzito ya kujadiri na usajili wa wapiga kura ambao wakati huu unafanyiwa pia mtandaoni.

Tume hii pia iliahirisha siku ya mwisho ya kukosoa daftari ya kura ambapo wapiga kura wana hadi tarehe 19 Julai kukosoa habari zao za vituo ambavyo watakuwa wakipigia kura.

Baadaye tume hii ya uchaguzi itachunguza habari hizi na kutoa orodha ya mwisho ya wapiga kura. Ambayo itakuwa muhimu kwa mipango ya mwisho ya upigaji kura.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.