kwamamaza 7

Tuko tayari kurudi nchini Rwanda, asema Jen. Kayumba Nyamwasa

0

Aliyewahi kuwa Kiongozi wa Jeshi la Rwanda, Jen.Kayumba Nyamwasa ametangaza yupo tayari kurudi nchini kwa njia ya amani kwani vita ni ghali na havijengi demokrasia wala maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa za chombo cha habari eNews nchini Zambia, Kayumba amesema haitakuwa rahisi kutimiza mpango wake wa kurudi nchini Rwanda na kuwa hana lengo la kupindua utawala wa Rais Kagame.

“ Inahitaji nguvu nyingi yunaposema kupitia njia ya amani. Tunapozungumza kuhusu amani, haina budi kujua ni njia ndefu na ngumu, Hilo ndilo jambo ambalo tunalifuata.”amesema Kayumba

“Inaweza kucuhua muda mrefu au mfupi lakini tuko tayari kuwa nchini kwetu. Siyo muhimu kupindua serikali, tunasema kuiweka nchi katika hali ya kidemokrasia.” Ameongeza

Kayumba alikimbia Rwanda mwaka 2010. Mnamo mwaka 2011, alihukumiwa na Mahakama ya jeshi nchini Rwanda bila kuwepo kufungwa jela miaka 24. Hukumu hii ni juu ya mashtaka ya kuhusika na vitendo vya ugaidi. Kayumba alikana mashataka yote kwa kueleza ni ya motisha za kisiasa.

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.