kwamamaza 7

Trump ashinda kura ya kuongoza Marekani, Clinton akubali kushindwa

0

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton, amempigia simu mpinzani wake Donald Trump wa chama cha Republican kukubali kushindwa katika uchaguzi wa rais.

Mapema usiku wa Jumanne mwenyekiti wa kampeni ya Clinton, John Podesta aliwataka mamia ya mashabiki walokusanyika katika ukumbi mjini New York kurudi nyumbani na kwamba mgombea wao hatazungumza.

[ad id=”72″]

Muda mfupi baadae mgombea mwenza wa chama wa Trump Mike Pence amewashukuru wafuasi na kumkaribisha rais mteule wa 45 wa marekani. Hii ikiwa ni tukio la kihistoria Marekani kwa mtu ambae hajawahi kushika nafasi au wadhifa wowote wa serikali kuchaguliwa kuliongoza taifa kuu la dunia.

Trump akiwahutubia wafuasi hao huko New York amesema Hillary amempigia simu na kumpongeza. Mfanyabiashara huyo ametoa wito kwa wamarekani wa pande zote kuungana na kufanya kazi pamoja.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.