Swahili
Home » Tanzania:Muigizaji wa filamu,Lulu kufungwa jela miaka miwili juu ya kifo cha Steven Kanumba
BURURUDANI

Tanzania:Muigizaji wa filamu,Lulu kufungwa jela miaka miwili juu ya kifo cha Steven Kanumba

Muigizaji wa fialmu,Michael Elizabeth aka Lulu/Picha:BBC

Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji wa filamu, Elizabeth Michale, maarufu kama ‘Lulu’, kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984,alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika michezo ya runinga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama ‘Bongo Movies.’

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msanii huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

Asili:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com