kwamamaza 7

Tafuta kujua tafsiri ya mavazi kutoka kuzimuni unayo yavaa (wanaume)

0

– Mavazi ya wanaume ambayo asili yake ni kutoka kuzimu katika viwanda vya kuzimu yapo mengi sana ila nitaelezea kwa kiasi fulani ili mpate picha na mpone.

– Mavazi yote yenye mambo za ajabu, mfano T-shirt inapicha ya mti wa bangi au sigara.

– Nguo yenye picha ufunguo- ina maana ule ufunguo umeivaa hiyo nguo ufunguo huo umekufungia usiende mbinguni na ufanikiwe kumkufuru mwenyezi MUNGU, na hata katika cheni, ukikuta kamaufunguo uelewe ni hatari tupu, hata cheni yenye msalaba ina maana uelewe unapovaa unakuwa wewe umelaaniwa na maisha yako yanasulubiwa katika ulimwengu wa roho. Pia uelewe hakuna msalaba mtakatifu kabisa hata ule aliouliwa nao YESU siyo msalaba mtakatifu ni msalaba wa laana na ndio sababu damu yake ilipomwagika pale msalabani ikatuondolea laana, sasa shetani akabuni njia nyingine na kuwapiga upofu watu waone msalaba ni kitu kizuri na kumbe siyo. Unajihukumu mwenyewe, hata kuzikwa na msalaba ni makosa.

Nikuulize swali unapozikwa je unaenda kuhukumiwa na wewe? Au je msalaba ni alama ya mkristo? Jibu siyo. Watumishi wanawapotosha watu kwa kumuamini shetani na kumfanya Yesu akose watu wa kwenda mbinguni. Jiulize swali kina Ibrahim, Isaka na Yakobo katika makaburi yaoipo misalaba? Jibu hakuna. Na kamasisi tu uzao wa Ibrahim, kwa nini tusiige mfano wa Baba yetu Ibrahim? Na zaidi je Yesu yeye alizikwa na msalaba? Jibu hapana, je Yesu si ndiye kweli na alionyesha njia ili tuifuate. Sasa swali, kama alionyesha njia, tuanze katika maisha yake je uliletwa msalaba? Jibu hapana. Sasa hii misalaba madhara yake unapokufa ukawekewa katika kaburi inakufanya wewe uliyekufa usulubishwe katika ulimwengu wa roho, na wote waliozikwa na misalaba wanateseka katika ulimwengu wa roho na shetani anamnyanyulia Mungu  si unaona msalaba wanataka wenyewe niwasulubishe na Mungu ni Mungu wa haki analiangalia neno lake, kataa kuzikwa na msalaba iga Yesu alivyozikwa, iga mazishi ya Ibrahim, Isaka na Yakobo, pamoja na mitume na manabii wa Mungu wa kweli waliopita ambao kwa heshima Mungu amewaita wazee 24. Kataa huo uchafu watu wanapotezwa, amenituma Yesu niwaeleze ukweli utakaye sikia utapona, utakaye kaza shingo damu yake haitamlilia Mungu katika mikono yake.

homme1

-Nguo zote zenye zipu kifuani tu, unapokuwa na nguo ya aina hiyo kila unapofungua zip unakuwa unayachana maisha yako katika moyo wako na unapofungua zipu hiyo unakuwa unayafungua usifanikiwe.

-Kila kitu chenye neno ultra kinatoka kuzimu.

-Mikanda yenye bastola au bunduki- unakuwa umevaa jini bedui katika maisha yako na makata hivyo wanayaharibu. Mikanda yote yenye sura za watu katika bacol au nembo yeyote ile uelewe umeivaa kuzimu na kuzimu inajiunganisha na wewe kupitia katika kitovu chako kwa njia ya bacol ya mkanda.

-Kusuka rasta- unakuwa umevaa pepo kichaa na mara nyingi huja kutokea katika mwili mtu anakuwa kichaa, na pia unakuwa na mambo ya freemason pasipokujua na wengine wanajua.

-Kuvaa suruali mlegezo- hiyo ni dalili wewe ni shoga katika ulimwengu wa roho na unapovaa hivyo unayaita majini yaliyokuoa katika ulimwengu wa roho yeye yazini na wewe.

-Kofia zote ambazo vijana wanasema ni za kileo zote zinatoka kuzimu na kijana anapovaa akili yake huibiwa ndoto zake zote hubakia boksi, na ndio sababu idadi kubwa ya wanaovaa hizo kofia fuatilia utakuta ni wavuta bangi, walaji wa cocaine, wahuni, wameharibika ni sababu ya hizo kofia zenye majina ya ajabu na ya wanamziki na watu ambao tayari ni wanachama wa freemason..

-Nguo za kubana kupitiliza mfano T-shirt, suruali, inakubana unayaonyesha maungo yako jinsi yalivyo.

-Kusuka nywele- unaposuka tayari uelewe wewe tayari  ni mke wa jini fulani kuzimu, na unaye mume unayemtumikia katika ulimwengu wa roho japo wanadamu hapa duniani wanakuwa ni wanaume tu ila ni boksi.

-Mashati yenye mipasuko katika sehemu za mifuko, mashati haya watu hawapendi kuyachomekea sababu yana mipasuko, sina haja ya kuelezea sana, yapokama Kaunda suti. Nguo yeyote ya mwanaume yenye mipasuko sehemu za kiunoni hizo zote ni za kuzimu, unapoivaa uchumi wako unapasuka na maisha yako yanakuwa ni ya shida shida tu.

-Nguo zenye sura ya nyoka, mamba, chui, madoa doa, viatu venye magamba au ukiviona vina sura ya magamba haijalishi ya aina gani havifai, ni viatu vya kuzimu.

-Viatu vilivyochorwa tick (Ö) au X ina maana hiyo tick unakubali jina lako liandikwe katika ufalme wa shetani na X ina maana maisha yako yanatiwa X yote.

– Kila kitu chenye jina MAX uelewe asili yake ni kuzimu na kina madhara.

-Viatu vyenye majina ya ajabu na vingi havielezeki hata sitaweza kuviacha kuandika even kwa 30 days, omba ROHO MTAKATIFU akufunulie wakati unahitaji viatu omba atakuongoza na roho ikigoma tu wacha, hiyo ni dalili.

-Kofia zote za duara zisizo na chepeo halafu zina kamba au kinaninginia unapozivaa, unakuwa umeweka kwato ya jini katika maisha yako na nyingine ni kofia za duara ile zimetobolewa mashimo mengi zote hizo ni makwato ya majini na shetani amewaletea wanadamu ili wawe wajinga na wasimjue MUNGU wa kweli siku zote za maisha yao, sasa uamuzi unao wewe utavaa makwato ya majini au utayatupa.

-Mwanaume anapovaa bangili (ringi) hapo unakuwa umejiingiza na kufunga ndoa na shetani, ila utakapoivua tu tayari umevunja ndoa na shetani, ringi hizi watu wengi wanafungulia vinywaji au kutumia kama silaha wakati wa kupigana na zaidi mwanaume hautakiwi kuvaa bangili katika mkono kabisa, unapovaa unafunga ndoa na shetani, na pia hata wengine wanafunga nyuzi katika mikono, hapo tayari umefunga ndoa na shetani na wewe ni mtu wa shetani, sasa amua, ila wengi wanajua kabisa ni masharti waliyopewa kuzimu inawezekana ni raia, mfalme, au mtu wa karibu, utashangaa siku zote ipo katika mkono, watu wanafikiri ni urembo, hapana hilo ni agano la shetani.

-Kutoboa masikio au sikio- iwe ni mtu yeyote yule wapo hata wachungaji wanatoboa masikio na kuvaa hereni- hao wote katika ulimwengu wa roho ni mashoga wala YESU hana ushirikiano nao. YESU hana mashoga. Jiulize hawa wanatokea wapi? Ni mashoga wanaoeneza injili ya yesu wa uongo na kuwapeleka watu kuzimu.

-Shetani aliwateka wengi hata waliookoka katika maeneo mbali mbali ila YESU amenituma niwaeleze ukweli sababu anaona mnavyoteseka na hampati majibu na akaniambia Hebron haya mateso yasingewapata wanadamu ila yamewapata sababu niliowaita wamemgeukia shetani na ndio anakuwa baba yao hivyo wanafanya kazi ya baba yao ambao ni lusifa hata wanangu wanateseka na kuangamia ila nimefurahi sasa sababu upo wewe Hebron, nimekupata wewe uliyenikubali kunitumikia na kuyatenda yale ambayo mimi na BABA yangu mbinguni na ROHO MTAKATIFU ndio tunayoyataka, na pia Hebron nataka uelewe kabla ya wewe kuumbwa MUNGU alishakuandaa na akajua ikifika muda wake atakusimamisha na anajua utaifanya kazi yake sababu anajua yeye aliyokuumba hivyo usiogope lolote. MUNGU alikuficha siku zote kama vile alivofichwa Musa akatunzwa na Farao hakuuwawa, hivyo ndivyo ilivyo kwako na utaifanya kazi yangu vizuri sana na kuzimu haitakuweza milele. Sasa nimefurahi sababu kila akusikilizaye na kubadilika na kutii unayowaeleza atapona sababu ndani yako MUNGU ameweka majibu ya viumbe vyote na kila kitu. Maneno haya kila nikumbukapo nasikia machozi yananitoka kwa ajili ya watumishi walivyomsaliti YESU hata na kugeuka freemason, wachawi, waongo, wanyang’anyi ila usiogope ninajua kinachokuja na watu mtamfurahia YESU WA NAZARETI.

-Haya magauni ya harusi ya kuzimu- kila gauni la harusi lenye kuburuza mkia- ina maana ule mkia unaoburuzwa ni mkia wa lusifa. Lusifa anao mkia ila nilimkata mkia wake. Unapofunga ndoa na gauni la jinsi hiyo ndoa yako unampa lusifa. Na unapovaa gauni la harusi unaonyesha mabega na manyonyo unakuwa unavaa gauni la pepo kuzimu la kufungia harusi zao na wewe unajiunganisha hivyo hivyo na mama wa makahaba. Ukiangalia leo hii watu ndio wanasema ndio fashion. Hii siyo fashion mimi nasema yote ili nisije nikaulizwa na YESU siku ile ya mwisho sikuwaeleza ukweli ili mpone na usijisumbue hata kama jina lake YESU linatajwa haiunganishi hiyo ndoa sababu la hilo vazi mimi pia nilikuwa sijui, ila sasa uelewe ili upone. Wanawake mkatae sasa msiwekewe tena mikia ya shetani ukauburuza.

-Kujipaka rangi ya kucha. Kila rangi inayo maana yake, rangi zote ulimwengu maana za kucha asili yake ni kuzimu. Ukipaka hizo rangi unaharibu maisha yako pasipo wewe kujua na hizo rangi zimechanganywa na rangi za ngozi za watu waliokufa baada ya kuchunwa ngozi zao na mashetani wakala nyama zao. Sasa unapozipaka unakaribisha majini katika maisha yako na uthamani wa mikono unaibiwa, hata pesa hazikai wala kazi zako hazibarikiwi sababu MUNGU hana mahali pa kupitishia baraka katika mikono yako sababu shetani ameshaweka vitu vyake katika mikono yako.

-Kucha za bandia- hizo ni kucha za majini walizozikata  kuzimu kama vile na wewe unavyokataga zako, unapozivaa kucha za bandia unakuwa unawapa majini  uthamani wa kucha zako ambapo katika kucha zako zipo Baraka wanaziiba zako unabakia na zao na unakuwa tayari umeingia urafiki na majini pasipo kujua japo wengine wanajua na wanayapenda majini.

-Nguo zote ambazo za wanawake zinakuwa na mipasuko zote hizo asili yake unakuwa unajitengenezea mkia wa lusifa na lusifa kuitumia njia hiyo kukupata.

-Nguo ambazo ni short ni fupi zinazoonyesha mapaja na hupendwa sana kuvaliwa na masecretary katika ofisi mbali mbali, sasa hilo vazi kila unapolivaa ina maana unamkubali shetani kabisa ila sasa uelewe haifai.

-Kuvaa pini katika ulimi, unapotoboa ulimi tayari unampa mama wa makahaba ulimi wako na vitu vyako kisha unabakia na ulimi wake na anakamata fahamu zako na kisha kwa kutumia ulimi huo uliovalisha pini anautumia kunyonya viungo vya siri vya kiume na mwanaume atakayefanyiwa hivyo anakuwa viungo vyake vimemezwa na Yezebeli katika ulimwengu wa roho kupitia mwili wa mwanadamu. Kazi kubwa ni kumeza viungo vya kiume kwa njia ya kuvinyonya na pia hata ukinyonywa ulimi au kiungo chochote na mtu aliyetoboa ulimi, uelewe anatumika kumeza vitu vya watu na ndani yake yupo Yezebeli na ndiyo sababu ametoboa ulimi. Ilikumjua mtu mwenye Yezebeli au Yezebeli anaishi ndani yake angalia ulimi ametoboa na katika ulimwengu wa roho na yeye anakuwa ni mtoto wa Yezebeli na Yezebeli anauhalali sababu anayo alama yake katika ulimi.

-Alama nyingine ya Yezebeli ni inayokufanya kuunganika katika kitovu cha mtu na Yezebeli utaona mtu anatoboa kitovu au anatoboa pembeni ya kitovu, hii ina maana  amejiunganisha kupitia kitovu, huyo mwanadamu atakuwa anatabia za kipepo, hata kutembea uchi, mlevi, hafai kuolewa au kuwa mke bora, sababu atakuwa ni kahaba.

-Na wengine wanatoboa (wanawake) wanakitoboa KISIMI wanakivalisha pini, yaani ukiona hivyo uelewe kile kiungo cha kike alicho nacho huyo binti siyo cha bindadamu ni cha pepo, kama alivyo mama wa makahaba na yeye amejitoboa na anavaa pin kubwa ya dhahabu ambayo ina urefu wa 30 cm na unene wa 2 cm. Mmh, haya mambo yanatisha kiasi hata mimi nimeandika huku nilikataa nisione alivyo ila YESU amenitia nguvu ili niwaeleze mjiepushe msifikiri ni vizuri hayo sasa yaelewe, okoka uvitupe hivyo vitu.

-Na alama nyingine ya mtu mwenye Yezebeli anavaa pini katika macho, bangili miguuni hasa bangili moja katika mguu mmoja na kujichora katika mapaja au kuchora moyo na alama ya mshale au kuandika majina ya watu katika mapaja au tumboni, mgongoni au popote katika mwili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.