kwamamaza 7

Taasisi ya utafiti yagundua virusi vya Zika nchini Tanzania

0

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania. Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.

Kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti huo, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya Zika.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Dkt Mwele Malecela ameambia BBC kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

“Bado tunajaribu kuangalia ni aina gani ya virusi vya Zika. Lakini hiyo ni dhahiri, tukizingatia kwamba mbu wanaoambukiza Zika wako nchini kwetu na mazingira yaliyoko nchini kwetu hayatofautiani sana na yale ya Amerika ya Kusini na nchi kama Thailand ambako ugonjwa huo unapatikana,” amesema Bi Malecela.

“Ugunduzi huu tumeupata kwa watu na tutaendelea kufanya kazi kuangalia kama tutaupata kwa mbu ambao utatuhakikishia basi kwamba ugonjwa huo ina maana umekuwepo nchini ni vile tu ulikuwa haujaonekana.”

Virusi vya Zika wamekuwa wakisababisha watoto kuzaliwa wakiwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo katika mataifa ya Amerika Kusini hasahasa Brazil. Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.