kwamamaza 7

Taarifa za tajiri raia wa Uganda aliyetekwa nyara akihifadhi fedha zake nchini Rwanda zaenea

0

Wasiwasi zimezuka mjini Katuna,wilaya ya Kabare baada ya tajiri kwa jina la Tweyogyere Justus kutekwa nyara na watu ambao hawajajulikana kwenye boda ya Rwanda na Uganda,Katuna alipo kuja kuhifadhi fedha zake kwenye benki nchini Rwanda.

Tajiri huyu maarufu kama ‘Mwana Muto’ yaani mwana mtoto anafanya kazi ya kubadilishana fedha za kigeni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mkurugenzi wa chama cha ushilika cha wabadilishaji wa fedha mjni Katuna,William Asiimwe ametanagaza kuwa Justus alitekwa nyara jana saa nane za mchana kwa upande wa Rwanda.

Diwani wa mji wa Katuna,Nelson Nshangabasheija amesema kuwa Justus alitekwa nyara baada ya kuhifadhi frw miliyoni 40 na kuwa alimpigia simu akipiga kelele kisha simu yake ikakaktika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Nelson amendelea kusema kuwa Mkurugenzi wa polisi kwenye boda,Zadoki Kagyeera pamoja na viongozi kutoka upelelezi nchini Uganda walijaribu kufanya ufuatiliaji lakini walinzi wa usalama kwa upande wa Rwanda wakakataa.

Taarifa za The Observer zinasema kuwa mkurugenzi wa polisi  wilaya ya Kabare,Dickens Bindeeba amesema kuwa suala hili litajadiliwa kati ya polisi wa Rwanda na Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hizi zinaendela kusema kuwa hii si mala ya kwanza tajiri raia wa Uganda kutekwa nyara akiwa nchini Rwanda kwa kuwa tajiri mwingine Dickson Tinyinondi maarufu kama Musalamu   aliuawa Januari, 2013 nchini Rwanda baada ya kupokonywa shilingi miliyoni 200 na mwenzake  Elvis Akandinda akauawa Februari 2012 baada ya kupokonywa fedha zake shilingi miliyoni 100.

Haya ni baada ya taarifa zilizoenea kuwa kuna vita baridi kati ya nchi ya Rwanda na Uganda juu ya upelelezi,kuwateka nyara wakimbizi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.