kwamamaza 7

Sudani Kusini: Kiongozi wa UNMISS yawapongeza majeshi wa Rwanda kwa bidii yao kwa kutoa msaada

0

Majeshi wa Rwanda waliyoko Sudani Kusini kwenye shughuli za kulinda amani wamepongezewa na Mkuu wa UN katika nchi hiyo kwa bidii wanayoonyesha kwenye shughuli hizo za kulinda amani katika eneo la kaskazini ya nchi hiyo.

Majeshi wa Rwanda 80 lwaliyoko katika shughuli za kulinda amani kwa ajili ya Umoja wa Mataifa, wamepelekwa hivi karibuni katika kijiji cha Aburoc kilichoko sehemu za Upper Nile, ambako kunakaa wakimbizi 2500.

Mjumbe maalum wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Sudan Kusini na ndiye Mkuu wa UNMISS, Amethibitisha kwamba kuweko kwa majeshi hawa kumesaidia kwa kiwango kikubwa wafanyakazi kuweza kuwafikia wakimbizi hawa na kuwaasilisha misaada kwao

[xyz-ihs snippet=”google”]Kwa mjibu ya tovuti ya UNMISS, Bw. Davis Shearer amekuwa akitembelea eneo hili katika mwisho wa wikendi hii kwa madhumuni ya kushuhudia hali ya maisha yawakimbizi hawa.

Rwanda ilipeleka majeshi kwa mara ya kwanza katika shughuli za kulinda amani Sudani Kusini (AMIS) mwaka wa 2004. Mwaka wa 2011, Rwanda ilishika nafasi ya kwanza miongoni mwa nchi zinazo majeshi wengi katika shughuli za kulinda amani. Nchi ya Rwanda imesifika sana kwa kuchangia katika shughuli za kulinda amani za umoja wa mataifa kwa kutoa majeshi yake. Mpaka sasa Rwanda ina majeshi katika nchi mbali mbali kama Mali, Sudani Kusini, Afrika ya Kati na Haiti.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.