kwamamaza 7

Sudan Kusini: Watu zaidi 50 wauawa kwenye mapigano

0

watu 56 wanaripotiwa kuuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka nje ya mji wa Malakal nchini Sudan Kusini.

Vikosi vya waasi viliendesha mashambulizi kwenye mji huo wa pili kwa ukubwa siku ya Ijumaa, baada ya kuteka vijiji vilivyo karibu.

Kwenye siku ya ijuma, waasi walisema kwamba wamekamata sehemu ya lalo na sehemu nyingine ya Wajwok na wanatarajia kuikamata Malakal.

[ad id=”72″]

Hata hivyo serikali inasema kuwa wanajeshi wake wamewatimua waasi hao hatua iliyosababisha maafa mengi.

Msemaji wa waasi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa wana matumaini ya kuteka mji wa Malakal na kuongeza kuwa hakuna matumaini ya kuwepo makubaliano kati ya kiongozi wao Riek Machar na rais Salva Kiir pamoja na kati ya kabila la Nuer na lile la Dinka.

Wiki zilizopita vurugu zimejiongeza sudan kusini na watu 60 waliuawa. Uongozi wa kijeshi pamoja na umoja wa kimataifa walisema kwamba raia walichomwa wakiwa na uhai.

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.