Swahili
Home » Suala la wakimbizi asili ya DR Congo kujadiliwa nchini Suitzerland
HABARI MPYA

Suala la wakimbizi asili ya DR Congo kujadiliwa nchini Suitzerland

Wakimbizi asili ya DR Congo wakati wa maandamano mwezi Februari/ picha na intaneti

Wizara ya Wakimbizi na Majanga nchini Rwanda (MIDIMAR) imetangaza hata kama wakimbizi  11,000 asili ya DR Congo katika kambi ya Kiziba wametangaza  kuwa na hiari ya kurudi kwao,suala hili litajadiliwa  nchini Suitzerland mwezi octoba 2018.

Afisa kwa wajibu wa masuala ya wakimbizi kwenye MIDMAR, Jean Claude Rwahama ametangazia vyombo vya habari uamuzi kuhusu hili suala haujachukuliwa bado.

“ Maelfu 11 walijiandikisha lakini utekelezaji wa mpango unahusu pande zote tatu yaani DR Congo, Rwanda na UNHCR.Tunasubiri uamuzi kutoka kwenye huu mkutano mwezi Octoba”

Rwahama ameeleza asilimia 99 za hawa wakimbizi ni wale kutoka Kambi ya Kiziba ambako kulitokea kutoelewana mwezi Februari 2018.

Kwa hilo, wakimbizi 11 waliaga dunia na maafisa wa polisi 7 wakajeruhiwa.

Kambi ya Kiziba iliwahudumu wakimbizi asili ya DR Congo 1720 tangu mwaka 1996.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com