kwamamaza 7

Suala la wakimbizi asili ya Burundi nchini Rwanda kujadiliwa mjini Geneve

0

Waziri wa Utawala wa ndani nchini Burundi, Pascal Barandagiye ameeleza kuna mpango wa kukutana na Rwanda kwa kuzungmzia suala la wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini Rwanda.

Huyu kiongozi amehakikisha hili litatokea mwezi ujao nchini Usuisi na linalenga kutafuta namna ya kuwarudisha hawa wakimbizi kwao.

Waziri Barandagiye katika hotuba yake tarehe 19 Septemba 2018 wilayani Ruyigi, alisema jambo hili linasubiliwa kwa hamu na Burundi.

“Alipokuja nchini Burundi,  Katibu Mkuu wa HCR alitoa ombi la mkutato wa pande tatu. Tunangoja kwa hamu hili. Inawezekana mwezi ujao kutakuwepo huo mkutano. Tuko tayari kuwepo kwa niaba ya faida zetu” Waziri Barandagiye alisema.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa ovyo tangu mwaka 2015 ambako viongozi wa Burundi walisema Rwanda iliunga mkono jambo la kuipindua serikali ya Rais Nkurunziza.

Hata hivyo, upande wa Rwanda ulilaani haya mashtaka kwa kusema masuala ya Burundi yanawahusu Warundi wenyewe.

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.