kwamamaza 7

Staff Sergeant Robert atupilia mbali tetesi kwamba Army Jazz Band imeanguka

0

Msanii Staff Sergeant Robert amesema kwamba anatupilia mbali tetesi zilizokuwa zikivuma zikisema kwamba kundi la Army Jazz Band limeanguka na kusisitiza kwamba wanakuja na minadi mpia.

Katika mahojiano na Bwiza.com, msanii huyu amesisitiza kwamba kundi hili lingali hai na linaendelea na shughuli za mziki na ni wakati ambapo kumekuwa na uvumi katika siku za hivi karibuni zikisema kwamba kundi hili limekwisha anguka na waliokuwa wanakundi wanaendelea na shughuli za mziki kibinafsi.

Amesema “ Watu wengi wanadhani tumeachana lakini siyo ukweli, ndio tumekuwa busy kwa kuwa hatuko tunazindua nyimbo kama awali. La hasha, kundi lingali hai mtashangaa katika siku za hivi karibuni, kwa upande wangu pia naendelea na shughuli za mziki niko na mradi wa albamu tatu, kila moja ikiwa na nyimbo nane, nitazifanya hizo zote chinichini, kuna mojawapo nilizowashirikisha Urban Boyz , na hata Jay Polly inayoitwa “funga butu”, kuna remix ya “sisi wenyewe” ambayo nitamshirikisha the Ben, niko baado na nguvu na hata Army Jazz Band tungali imara”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Sergeant Robert

Aidha alisema kwamba wakati ambapo hayuko kwenye kazi huwa kwenye familia yake au kwenye maombi kwa kuwa siku hizi aligeuka mlokole maana anashinda wakati mwingi kwenye kanisa ama kujifunza biblia na hii inasababisha watu kufikiri kwamba amepotea.

Army Jazz Band ni kundi lililoanza mwaka wa 1999 likiundwa na wanajeshi. Walitunga nyimbo nyingi zikiwemo za amani, za uzalendo na kadhalika.

Ingawa wanaunda kundi moja, kulitokea wakati Sergeant Robert akazindua nyimba za kibinafsi ikiwemo impanda na weekend ambazo zilikuwa mashuhuri.

Richard wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.