Swahili
Home » Staff aliye husika na upelelezi na kuandaa vita vya FDLR amerejea Rwanda
HABARI MPYA

Staff aliye husika na upelelezi na kuandaa vita vya FDLR amerejea Rwanda

Major Mvuyekure Pierre aliye husika na upelelezi pia kuandaa vita ndani ya kundi ya wanamgambo wa FDLR katika Kivu ya kasikazini amerejea Rwanda tarehe 25 Novemba 2016.

Maj Mvuyekure ni mwenye ukoo wa Nyabihu na aliachana na luteni wa kwanza Ntibibuka Olivier mwenye ukoo wa wilaya ya Gakenke huko Nemba, na alihakikisha kwamba hataambatana tena na jeshi la Congo (FARDC ambalo hufanya kazi Masisi.

Maj Mvuyekure aliye julikana kwa jina la Kinyange alikuwa akiishi sehemu ya Nyamuragira, kurejea kwake ilikua ndoto zake ambazo zimefanya muda wa miaka miwili ambazo zimetimilika.

Aliendelea na kusema kwamba alikua na kazi nzuri ya kuandaa vita ila asema kwamba hata walikua wakifanya hayo aliona kwamba wanachoka bure kwa kua hawangelishinda vita kama vile alisema kwa lugha ya kifaransa “mission impossible”, yamaanisha yasiyowezekana na tarehe 19 novemba ndipo alibahatisha kutoha mahali alikuwepo na kuwaendea MONUSCO huko Tongo ili afikishwe Goma na kurejea.

Aliambatandana na FDLR munamo mwaka wa 1997 wakati wa vita ya majambazi na alishikwa pamoja na wengi, wakapelekwa Congo na huko ndipo alipewa mafunzo ya Kijeshi.

Luteni wa Kwanza Ntibibuka Olivier naye hivyo alitwaliwa na majambazi wa FDLR mwaka wa 1998, hata kama alifundishwa mambo ya vita na akafanya kazi pamoja na FARDC hakufurahia kuitumikia taifa lingine alikua amechoka na ndipo naye akaamua kuja kuitumikia nchi yake.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com