kwamamaza 7

SOS Burundi yahakikisha kunaandaliwa mpango wa kushambulia Rwanda

0

Shilika la SOS Burundi limehakikisha kuna mpango wa kushambulia  Rwanda unaoandaliwa nchini Burundi.

Ukuta wa Facebook wa hili shilika unaeleza serikali ya Burundi ilidanganya raia wake na nchi nyingine ilipoungana nao mkono kwa kuwatafuta wanamgambo inayosema kuwa wanajificha katika msitu wa Kibira,wilayani Mabayi na Bukinanyana  tarehe 21 Juni mwaka huu.

Mmoja mwa vijana ambaye ni mkazi wa eneo hili, ametangaza  hawa wanamgambo wanaishi hukokwa miezi miwili wakiwa na vifaa vya kijeshi wanavyopatiwa na bataliyani ya 112  ya jeshi la Burundi.

Kuna taarifa kwamba viongozi wa hawa wanajeshi wa Wanyarwanda ambao Warundi wanawaita “ Interahamwe” wanaishi hotelini ya eneo la Ndora.

Hizi taarifa zinaeleza wakazi wamejawa na hofu la vita vinavyoweza kuzuka huko na wameanza kutoka katika hili eneo kuelekea wilayani Mabayi.

Mmoja wao alisema” Tulikuenda huko mwituni tukiwa na polisi,wanajeshi ila hatukuwaona wanamgambo kwa kuwa walituambia kubeba vyakula na tulipofika msituni wakatuambia kurudi nyumbani”

Kwa upande wa Burundi, Kiongozi wa jeshi hii operesheni wilayani Mabayi na Bukinanyana amekataa kuongea kuhusu madai ya hawa wakazi.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.