kwamamaza 7

Soma ujumbe wa rais Kagame kwa rais mwenzake wa Burkina Faso uliowashangaza wengi.

0

Ujumbe Kagame aliomwandikia mwenzake Kaboré ulikuwa kwa ajili ya kumshkuru rais huo wa Burkina Faso kwa kumpongeza kuwa ameshinda uchaguzi.

Rais wa Burkina Faso, Kaboré ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa lugha mbili akimpongeza rais Kagame kwa ushindi alioupata wa kuitawala Rwanda kwa muhula mwingine.

Baada ya Rais Kaboré wa Burkina Faso kuandika ujumbe huo Kagame naye hakuchelewa kumjibu mwenzake naye kwa Lugha mbili yaani Kiingereza na Kifaransa.

Kagame aliandika “It is much appreciated. Merci mon frère Kaboré, yaani Ni la kufurahia mno. Ahsante ndungu yangu  Kaboré”,  ujumbe uliowashangaza wengi.

Mazungumzo ya marais hao

Si mara nyingi watu wanamskia Kagame akiongea ama akitumia Kifaransa kwa namna yoyote na anapojaribu kuna watu ambao wanalichukua  kama jambo la kushangaza.

Kagame kwa nyakati zake za mwanzo za utawala alikuwa akipata taabu kuongea na hata katika Kinyarwanda lakini kwa sasa unaweza ukasema yeye ni hodari wa lugha hiyo.

Mbali na rais huyu Kaboré aliyemtumia ujumbe wa kumpongeza rais Kagame kuna marais wengine waliochukua muda kumpongeza rais Kagame kwa kuchaguliwa kwa muhula mwingine wa kuitawala Rwanda. Marais hao ni Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye atakuwa akisubiri ikiwa atakuwa mshindi wa uchaguzi wa kesho ambao anakabiliwa na ushindani mkali wa hasimu yake Laila Odinga, mwingine ni John Pombe Magufuli wa Tanzania, mfalme wa Oman, rais wa Sahara ya Magharibi Brahim Ghali na viongozi wakuu wengineo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.