Swahili
Home » Sikubaliana na Tume ya Uchaguzi ingawa sijakata tamaa -Diane Rwigara amwambia Balozi wa Marekani
BIASHARA SIASA

Sikubaliana na Tume ya Uchaguzi ingawa sijakata tamaa -Diane Rwigara amwambia Balozi wa Marekani

Diane Rwigara ambaye ni mgombea kike pekee aliyetangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais wa Rwanda, baada ya kumkuta Erica J. Barks-Ruggles, balozi wa Marekani, amefunguka kuhusu kile walichozungumza.

Ni katika mahojiano na vyombo vya habari, Ijumaa tarehe 30 Juni, alipotangaza pingamizi alizokuwa nazo ambazo zilimzuia kutangazwa miongoni mwa wagombea walioidinishwa kwa muda.

Akigusia kile walichozungumza na balozi alisema “tulikuwa na mazungumzo ya pamoja na aliniuliza kauli yangu kutopatikana kwenye orodha ya wagombea waliotangazwa halali kwa muda. Alikuwa anataka kujuwa pingamizi zipi zipi na kutaka kujua kwamba angeshughulikia kuhusu suala hilo na ngazi husika”

Watangazaji wa habari walimhoji juu ya pingamizi zilizomkabili na kumfanya kutotangazwa miongoni mwa wagombea walioidinishwa kwa muda

Rwigara alisema kwamba alishangazwa sana na jinsi Tume ya Uchaguzi ilivyosema hakukidhi idadi za saini za wafuasi ikiwa alikuwa amezidisha idadi aliyokuwa anatarajiwa kuwa nayo ya wafuasi 660 na kuwa na idadi ya saini 985.

Jambo jingine lililomtia mashaka ni kuwa katika wilaya ya Kicukiro hakuwa hata na saini moja ya mfuasi iliyokubaliwa na kuongeza kwamba kuna raia mmoja anayemjua kwa karibu ambaye saini yake hakukubaliwa ingawa Rwigara yeye anamwamini kuwa anakidhi vigezo vyote vinavyohitajika kukubaliwa.

Hata hivyo, Rwigara alimwambia Balozi Ruggles kwamba hakuelewana na Tume ya uchaguzi na kuongeza kwamba hakukata tamaa na ataendelea kuzisaka saini za wafuasi. La hasha alikuwa ikionyesha hali ya kutojiamini katika matamshi yake kwa kusema “ tutaendelea kuzisaka saini za wafuasi wa ziadi ingawa hatujui nani atakubaliwa na nani hatakubaliwa”

Wengi wa waliompigia saini walitofautishana saini zao na zile zilizoko kwenye kadi ya Utambulisho.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rwigara alisema kwamba wanatarajia kile ambacho Tume hii itawatangazia kuhusu kauli ya ugombea wao tarehe 7 Julai ambapo orodha ya mwisho ya wagombea itatangazwa.

Ni mara nyingi Rwigara aliposikika akaishtumu Tume hii kutokuwa huru kwamba kuna madai aliyoikabidhi kuhusu pingamizi alizozikuta na Tume hii kutofanya kitu.

Diane alisema kwamba kuhusu ktambulisho cha uraia, kulikuwa na dosari fulani kuhusu uraia wa asili wa mmoja ya wazazi wake ambayo nayo imekwisha kosolewa.

Mpaka sasa wagombea waliokwisha idinishwa kwa muda ni 2 ambao ni rais Paul Kagame aliyepita kwa tiketi ya RPF na Dkt. Frank Habineza wa Chama cha Green.

Wagombea binafsi wote ambao ni Mwenedata Gilbert, Mpayimana Philippe na Barafinda Sekikubo Fred walihimizwa kuzitafuta nyaraka ambazo zingali zinakosekana hadi tarehe 6 Julai ambayo ni makataa ikiwa wagombea rasmi watatangazwa tarehe 7 Julai.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com