Swahili
Home » Siku ya tano ya kampeni ya mgombea wa RPF Paul Kagame- yaahidi maisha bora
HABARI MPYA SIASA

Siku ya tano ya kampeni ya mgombea wa RPF Paul Kagame- yaahidi maisha bora

Mapambo kwenye kilima

Leo tarehe 18 mwezi Julai ambayo imekuwa ni siku ya tano ya kampeni kwa wagombea kiti cha urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Mgombea wa chama tawala cha RPF, ameendelea ziara yake ya kampeni kwenye wilaya ya Ngororero na wilaya jirani ya Muhanga.

Alianzia shughuli zake za kampeni katika wilaya ya Ngororero ambako kumekuwa na wananchi kwa wingi wa kupita kiasi na waliomkaribisha kwa shangwe wakiimba nyimbo za kumsifu wakimwonyesha kwamba wanamwunga mkono katika uchaguzi unaofanyika mwezi ujao.

Kulitolewa ushahidi wa mwananchi aliyejiendeleza kufuatia utawala wa chama cha RPF. Mwananchi huo anayetambulika kwa jina la Mujawayezu Laurence amesema kwamba licha ya kuwa alikuwa pamoja na wanamgambo walio misitu ya Kongo alirejea nyumbani na kupewa msaada mnono kutoka kwa serikali inayotawaliwa na chama cha RPF.

Lililomshangaza mno ni kuwa alijikuta akiolewa na mume ambaye ni mwanajeshi wa RPF. aliendelea kwa ushahidi wake kubainisha kwamba aliweza kujiendeleza kufuatia sera nzuri za RPF na kwamba kwa sasa yuko kwenye hatua nyingine kimaendeleo.

 

Kagame alianza kwa kuwashkuru wananchi na wanavyama wa vyama wenza vinavyomwunga mkono kwa kuja kumwunga mkono.

“ nawashkuru wanachama wa RPF waliko hapa na wanavyama wenza waliokuja kuunga mkono chama cha RPF  kwa kuwa kwa umoja hatutashindwa lolote. Tunapajua tulipotoka ,tulipo na tunapoelekea lakini lengo la pamoja ni kufika mbali na kwa kasi”

Aliendelea “hakuna lingine litakalotusaidia kujiendeleza isipokuwa kujiweka pamoja. Sisi wote tuna lengo moja kwenye tarehe 4”

Paul Kagame aliendelea kuwahimiza kumpa kura ili waendelee na maendeleo kwenye ngazi zote na kuendelea kuijenga nchi yenye misingi ya maendeleo imara.Hapa aligusia kuhusu elimu ya watoto kwamba itatiliwa nguvu.

Alisema kuhusu pia miundombinu kwamba watafanya kila juhudi kuusaambaza umeme hadi kwa asilimia 90 ya wananchi. Kagame pia aliahidi kushughulikia suala la lishe kwa kuhakikisha wananchi wa afya bora kwani ndio ishara ya maendeleo.

Baada ya kukamilisha shuguli zake hapo wilaya ya Ngororero ambako kulionekana kwamba walikuwa wamefanya maandalizi ya juu kwa kupamba mahali pote hadi kwenye vilima aliendelea kwenye wilaya ya Muhanga.

Mapambo kwenye kilima

Rais kwenye wilaya ya Muhanga- Picha

alipofika wilaya ya Muhanga kulikuwa na maandalizi yaliyopewa jina la harusi  kwa mapambo yaliyokuwa si ya kawaida na hapa Paul Kagame akasisitiza kuwa ni sherehe kweli kweli itakasherekewa rasmi tarehe 4 na ambayo itaashiria kujiunga pamoja kwa kuafikia malengo ya maendeleo

Akitembea kuwasalimu

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com