Swahili
Home » Siku ya 14 ya Kampeni kwa wagombea Urais wa Rwanda
HABARI SIASA

Siku ya 14 ya Kampeni kwa wagombea Urais wa Rwanda

Jana tarehe 27, imekuwa ni siku ya 14 kwa wagombea urais wa Rwanda ambapo Paul Kagame wa RPF amekuwa akijiunga na wananchi wa Rutsiro kwenye kampeni zake huku Mpayimana Phillipe akiwa kwenye wilaya za Kirehe, Ngoma , Kayonza, Rwamagana na baadaye wilaya ya Kicukiro mjini Kigali.

 

Walichosema wagombea

Paul Kagame

Mgombea huyu wa chama cha RPF ambaye anawania muhula wa tatu wa urais wa Rwanda amekuwa akiendesha kampeni zake wilaya ya Rutsiro ambapo amewaambia wananchi wa pale kwamba licha ya maendeleo waliyoyafikia wajuwe “mema hajafika bado”

Hapa aliwaahidi mengi wananchi wa Rutsiro yakiwemo kunufaika na migodi inayokuwepo wilaya hiyo na hata ziwa Kivu wanalopakana nalo.

Hakukosa pia kuwagusia vijana kwani ni nguvu za nchi na kwa kuwa wanachukua asilimia nyingi ya wanyarwanda wanapaswa kuimarishwa na kuandaliwa kama nguvu za kesho kwa kupewa elimu bora na mengine.

 

Mpayimana Phillipe

Akiwa Kayonza

Mpayimana Phillipe ambaye ndiye mgombea huru pekee katika uchaguzi wa mwezi ujao ameendesha kampeni zake kwenye wilaya nne ikiwemo Ngoma, Kirehe, Rwamagana na Kayonza na hatimaye Rwamagana.

 

Mpayimana amesema iko mipangoni mwake kusambaza maji karibu na makazi ya kila mnyarwanda na kwa hivyo hakuna yeyote atakayelazimu kwenda kuchota maji.

Akigusia kuhusu wakazi wa Kirehe amesema kwamba atahakikisha maji ya mto Akagera anasafishwa na kutumiwa.

Kuhusu hoja ikiwa atapunguza ada ya maji kwa wakazi wa eneo hilo linalokumbwa na uhaba wa maji amesema kuwa maji yatakuwa bure kwani hakuna raia anayestahili kulipa ili kupata maji.

Amewaahidi wakulima pia kwamba atawasaidia kupata masoko ya kuuzia mavuno yao na kwamba atatafuta na hata nje ya nchi.

Frank Habineza

Frank Habineza ambaye ni mgombea kwa tiketi ya chama cha Green yeye amekuwa akiendesha Kampeni wilaya ya Kamonyi na Ngororero ambako ahadi zake ziligusia kuilinda mazingira na hata kuboresha maisha ya wanyarwanda

Kuhusu mazingira amesema kwamba atapanda miti kwenye ng’ambo za mto Nyabarongo na kwamba kuhakisha maji hao yanatunzwa vizuri na hata ananufaisha wa kazi wa maeneo ya karibu na mto huo.

Mgombea huyu alisema vile vile kwamba ataweka mipangoni mwake mfumo wa kijenga vituo vya afya na hospitali vya kukidhi wadumiwa wa wa sekta ya afya na hata kuhakisha mfumo wa bima ya jamii wa “mutuelle de santé unatumika vizuri na wanyarwanda wote wanapata huduma sawa za kiafya.

Amesema kwamba ataongeza pia mishahara ya waalimu,walinda usalama na hata kuweka mshahara wa msingi kwa wafanyakazi. Aliongeza  kwamba pia ataweka mfumo wa kuwapatia wanafunzi chakula wakiwa shuleni.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com