kwamamaza 7

Siku ya 10 ya Kampeni za Frank, ahaadi kuibadili Kibeho eneo la aina yake la utalii duniani

0

Siku ya jana ambayo imekuwa ni siku ya 10 ya kampeni kwa wagombea wanaowania kiti cha urais wa Rwanda  katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao. Frank Habineza ameendesha kampeni zake wilaya ya Nyaruguru na Huye kushindwa kufanyika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Dkt.Frank Habineza ambaye ni mgombea kwa tiketi ya chama cha Green akiwa pale kwenye kampeni ameahidi kubadili mengi ikiwemo kuimarisha sekta ya miundombinu na hata kuibadili Kibeho, mahali panapofahamika kama “ardhi takatifu”, eneo la aina yake la utalii kama taarifa hii kutoka gazeti la New Times inavyoeleza.

Eneo la utalii la Kibeho limepewa jina la “ardhi takatifu” kufuatia ujio wa Bikra Maria.

“Tumejariwa kuwa na ardhi hii takatifu lakini kunahitajika juhudi za kuifanya rahisi kufikiwa kwa kutengeneza mabarabara na vitu vingine muhimu vitakavyowezesha watalii kuvutiwa na eneo hili” asema

Amesema kuwa atahakikisha kuwa mahali hapa panaingia kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Amesema pia kuwa atalegeza kamba kuhusu masharti ya kupiga marufuku mavazi ya sekeni yaani “chagua” hadi serikali itakapokuwa na uwezo wa kutengeneza nguo za kufaa soko la ndani na kwa bei isiyo ya juu kwa wananchi.

Mgombea huyu hakuendesha kampeni zake kwenye wilaya ya Huye kama ilivyokuwa inatarajiwa na ametoa misingi ya tekniki kama alivyoeleza.

Siku ya leo tarehe 24 anatarajiwa kuwa atakuwa akiendesha kampeni zake kwenye wilaya ya Bugesera na kesho atakuwa kwenye wilaya mbili ambazo ni Kayonza hatimaye Rwamagana.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.