kwamamaza 7

Shyogwe:Miaka nenda rudi yapita mlowezi akisubiri kujengewa nyumba

0

Mlowezi wa kijiji cha Musezero,tarafa ya Syogwe,Minani Evariste anatimiza miaka 4 akingoja msaada wa kujengewa  nyumba aliyekubaliwa na serikali mwaka 2013.

Nyumba yenye chumba kimoja aishimo Minani na familia yake

Minani Evariste alikubaliwa kujengewa nyumba baada ya kwake kuharibika kipande kimoja na kwa sasa yeye na familia yake ya mke na watoto wawili wanaishi katika kipande kilichobaki chenye chumba chumba kimoja cha kulalia.

Minani amesema kuwa a alipigwa  picha na kusaini kuwa atajengewa nyumba  kutoka miaka 4 iliyopita hadi leo na kuwa anaishi hali mbaya kwa kuwa hana uwezo wa kujijengea nyumba mwenyewe kupitia kazi yake ya ufinyanzi wa vifa vya kienyeji kwa kusema”waliniita kwe na kunipiga picha na kusaini kuwa nitajengewa nyumba kule Rukaza lakini siku nenda rudi sijapata”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akieleza kuhusu madai,katibu mtendaji wa tarafa la Shyogwe,Habinshuti Vedaste alisema kuwa hajui tatizo la Minani kwa kuwa yeye ni kiongozi mpya wa tarafa hii ,Habinshuti amesema”Sijui tatizo la Minani lakini nitafanya lolote kujua habari zote kuhusu tatizo hili”.

Kiongozi huyu amesema kuwa wanataka kumushauri Minani kwa kuwa ana nguvu za kufanya kazi ili kujitunza na kuwa inabidi mtu fulani  mwenye uwezo wa kujenga nyumba za mtindo wa mjini kumbadilishia makazi ili naye apate panapolingana na uwezo wake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.