Swahili
Home » Shilika la OLUCOME lawataka Rwanda na Burundi kufuata nyayo za Ethiopia na Eritrea
HABARI MPYA

Shilika la OLUCOME lawataka Rwanda na Burundi kufuata nyayo za Ethiopia na Eritrea

Shilika la kupambana na rushwa na matumizi ovyo ya mali ya umma (OLUCOME) limewata Rwanda na Burundi kufuata nyayo za Ethiopia na Eritrea katika ushilikiano.

Shilika hili limetangaza haya baada ya Ethiopia na Eritrea kutia saini mkataba wa ushirikiano baada ya miaka mingi wakiangaliana kwa jicho la chui.

OLUCOME kupitia twitter imetangaza Rwanda na Burundi wanastahili kushirikiana kama walivyofanya Ethiopia na Eritrea.

“Kwa nyayo za Ethiopia na Eritrea, tunaomba Rwanda na Burundi kufuata hizi nyao kwa mema ya kibiashara” OLUCOME wameandika

Ushirikiano kati ya Rwanda ulianza kuwa mkia wa mbuzi mwaka 2015 baada ya Burundi kushtaki Rwanda kuwa iliwaunga mkono wanajeshi waliojaribu kupindua serikali ya Rais Nkurunziza tarehe 13 Meyi 2015

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com