kwamamaza 7

Shilika la haki za binadamu,HRW lanyoshea kidole tena serikali ya Rwanda

0

Shilika la haki la za binadamu,Human Rights Watch leo tarehe 29 Septemba 2017 imeweka wazi kwamba serikali ya Rwanda imendelea kutesa haki za wapinzani wake baada ya uchaguzi wa rais.

Kupitia tangazo lake,kiongozi wa HRW mwa Afrika ya kati,Ida Sawyer ameleza kuteswa kwa wapinzani wa serikali ya Rwanda ni ishara ya kuwa serikali haiko tayali kusikiliza wanaoikosoa au mchango wa vyama vya upinzani.

Kiongozi wa HRW mwa Afrika ya kati,Ida Sawyer

Ida Sawyer amendelea kusema kuwa vitendo vya serikali ya Rwanda vya kuwatesa wapinzani wakiwemo Diane Rwigara,familia na wafuasi wake na viongozi wa chama FDU-Inkingi ni ujumbe kwa yeyote anayetaka kubadilsha mambo.

Diane Rwigara alipokamatwa na polisi siku zilizopita

Pia,HRW linaeleza kwamba hata kama wapinzani hawana nguvu,walikomeshwa kuwania katika uchaguzi wa rais isipokuwa wawili yaani Phillipe Mpayimana na Frank Habineza walioteswa na kubabaishwa wakati wa uchaguzi.

HRW imetangaza haya baada ya baraza la vyama 11 nchini Rwanda (NFPO)jana kupitia spika wake,Mhe.Clotilde Mukakarangwa kutangaza kwamba wanafurahia  ulivyoendelea uchaguzi wa rais.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na hayo,HRW inatangaza kuteswa kwa Diane Rwigara baada ya sauti zilizotiwa nje ambapo kunasikika mpango wa familia ya Diane Rwigara kuipindua serikali ya Rwanda na baada ya kundi la viongozi wa chama cha FDU-Inkingi kuhukumiwa mwezi kizuizini kwa kuwa na hatia za vitendo vya ugaidi.

Wanachama wa FDU-Inkingi walipokuwa kizimbani

HRW imependekeza kwamba serikali ya Rwanda kutohusisha mambo ya mahakamani na  faida za kisiasa na kuwapa haki zao wapinzani bila kuegamia upande.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Si mala ya kwanza HRW kuweka wazi ripoti ambazo serikali ya Rwanda inakana kwa kueleza kuwa ni kinyume na mkataba.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.