kwamamaza 7

Serikali yatangaza mpangilio wa uchaguzi wa rais 2017

0

Serikali ya Rwanda imetangaza tarehe za uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao. Kulingana na tangazo lililotolewa baada ya kikao cha baraza la mawaziri, uchaguzi huo utafanyika tarehe 4 Agosti 2017.

Wanyarwanda wanaoishi nje watapiga kula kabla, yaani tarehe 03 Agosti 2017. Saa za uchaguzi itakuwa kuanzia saa moja za asubuhi hadi sa tisa mchana.

Shughuli za kampeni zitaanza mwezi Julai lakini hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kwa wagombea kuwasilisha hati za kugombea urais, licha ya kwamba tangazo hilo linasema wagombea watatangazwa kabla ya kuanza kwa kampeni.

[ad id=”72″]

Mtu pekee katika kambi ya upinzani aliyetangaza nia yake ya kugombea urais ni kasisi wa zamani wa kikatoliki Thomas Nahimana. Hata hivyo juhudi zake za kutaka kurejea nchini Rwanda wiki mbili zilizopita ili kuandikisha chama chake na kugombea urais ziligonga mwamba.

Kasisi Thomas Nahimana na wenzake watatu walikataliwa kuingia nchini Rwanda walipokuwa mjini Nairobi Kenya kuelekea Rwanda kutoka nchini Ufaransa anakoishi kama mkimbizi.

Inategemewa kuwa mshindi wenyewe wa uchaguzi wa atatangazwa kabla 16 Agosti 2017. Bajeti itakayotumiwa itakuwa bilioni 5,4.

[ad id=”72″]

Vyama vya siasa nchini Rwanda havijaonyesha jitihada za kushindania urais. Waziri wa zamani wa usalama Sheh Musa Fazil Harelimana alipokuwa kiongozi aliwahi kusema kwamba chama kinachomhifadhi cha PDI hakiwezi kumtoa mshindani mwingine kama Paul kagame kutoka chama cha Uongozi RPF Inkotanyi anakuwepo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.