Home HABARI Serikali yaonya wafamasia wanaouza dawa ya malaria kwa wagonjwa wasio na vyeti vya daktari
HABARI - SIASA - June 22, 2017

Serikali yaonya wafamasia wanaouza dawa ya malaria kwa wagonjwa wasio na vyeti vya daktari

Wizara ya Afya imepiga marufuku maduka ya dawa yanayouza dawa kali kama (Coartem) ya malaria kiharamu.

Wizara iliweka taratibu za kuuza dawa kama hizi ambapo maduka yanapaswa kuwaomba wanunuzi kuonyesha vyeti vya madaktari lakini wachache huheshimu kanuni hizi.

Dkt. Uwimana Aline Mkurugenzi wa Taasisi ya Kutoa Matibabu ya msingi dhidi ya malaria (Director of Case Management Unit) katika Idara ya Nchi ya Afya(RBC) ametangaza,katika mahojiano na RBA, kwamba aonya maduka yanayouza madawa kwa namna hii. Hii ni baada ya raia mmoja kulishtumu duka fulani kuuza dawa kiharamu

“ tunawalaumu wanamaduka wanaozuza madawa ya malaria kiharamu. Dawa ya malaria inatolewa kufuatia cheti cha daktari. Wajue kwamba jukumu lao si kutibu bali kuuza dawa ambazo wagonjwa walizopendekezwa kununua.” asema

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amegusia pia juhudi za serikali kupigania afya bora ya wanyarwanda kwa kuwaweka washauri wa afya nchini kote, vituo vya afya na hata vituo vidogo ambavyo watu huweza kutoa huduma za msingi.

Alisema zaidi kuwa hukuta maduka yanayouza maduka kiharamu huwa pia na bei ya juu ya ile iliyo halali.

Mfamasia Nteziyaremye Jeremie ambaye amezungumza na Bwiza.com amesisitiza kwamba kosa hili ambalo amelikuta katika madukada kadhaa aliyoyatembelea ni la kuchukuliwa kwa makini.

“Kila mteja anayekuja kununua dawa hususani kali tunamwomba kuonyesha cheti cha daktari , hayo ni kwa mjibu wa taratibu zilizowekwa na wizara ya afya na tunayafuata, tunapoona ana tatizo jingine tunampeleka kwa daktari tena”

Kwa kuwa wahudumu wa maduka hayo huwa ni watu wataalam wa mambo hayo hawangefanya kosa hilo.

Tulipomwuliza ikiwa hawangemchukua mitahani kabla ya kumpa dawa amesema kwamba Maduka ya Dawa ana mambo yanayoruhusiwa kufanya na yale ambayo ni marufuku kwa vile kuchukua mitihani ya malaria ama kudunga sindano.

Maduka ya dawa ana ruhusa ya kuuza madawa ya magonjwa madogo kama kuumwa na kichwa, madonda lakini kwa magonjwa kali ni marufuku

Wafurumasia pia wanaruhusiwa kisheria kuuza madawa ya aina ya OTS (Over-the-Counter Medicines) ambayo anapunguza maumivu, kutibu meno, na hata maumivu ya misuli haswa kwa wachezaji lakini hawaruhusiwi kuuza madawa ya aina ya “antibiotic”

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.