kwamamaza 7

Serikali ya Uholanzi yapiga marufuku ombi la wabunge la kukoma kuisaidia Rwanda

0

Serikali ya Uholandi imewanyamazisha wabunge walioandika wakiitaka serikali kukoma kuisaidia  Rwanda kutokana na mkataba kati yake na Arsenal.

Wabunge wakiwemo Joel Voordewind na Isabelle Dicks waliandikia  Waziri wa Uchumi wa Kimataifa na Ushirikiano wa  Maendeleo, Sigrid Kaag wakimuuliza kama wakimuuuliza wanavyochambua nchi wanayosadia iliyosaini mkataba ghali na timu yajiri duniani ya Arsenal.

Waziri Saag amewajibu wabunge kuwa hawezi kuhakikisha kama  Rwanda italipa $ miliyoni 40 kwani alijua haya mambo kupitia twitter na vyombo vya habari na kuwa haikutangazwa rasmi na baadhi ya viongozi wa Rwanda.

Waziri wa Uchumi wa Kimataifa na Ushirikiano wa  Maendeleo wa Uholanzi, Sigrid Kaag

“Rwanda ingali baadhi ya nchi fukara ila ina lengo la kuacha kutegemea. Huu nimwelekeo mzuri wa uchumi na iwekezaji kama ule wa Uholanzi”Waziri Kaag amefafanua.

“ Serikali itaendelea kushirikiana na Rwanda kwa mambo ya vyakula, usafi na maji,usalama.Tunataka kuendelea na huu ushirikana huu mwaka wa 2018” ameongeza

Waziri Kaag amesisitiza Rwanda kujitegemea haina budi  kutumia maendeleo ya kiuchumi.

“Uholanzi unaelewa kwamba Rwanda inatafuta mbinu pana za kupiga hatua ya mandeleo kupitia utalii.Kuchagua Arsenal linahusu Rwanda peke yake”

Jezi za Arsenal zenye ujumbe “Visit Rwanda

Haya ni baada ya Wabunge nchini Uholanzi kukosoa mkataba wa Rwanda na Arsenal wakieleza sio jambo la kujivunia Rwanda kusaini huu mkataba wa bei ghali wakati ambapo dunia nzima inapambana na ufukara.

Serikali ya Rwanda ilitangaza huu mktaba unalenga kuleta maendeleo ya utalii, na maendeleo ya kandanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.