Swahili
HABARI MPYA

Serikali ya Uganda yaeleza “ Hatukufunga watu kwa kuwa ni Wanyarwanda”

Serikali ya Uganda imeeleza haikuwafungwa watu kutokana na kuwa ni Wanyarwanda.

Haya ni baada ya madai kwamba Uganda inawafunga watu asili ya Rwanda ambao waliwahi kuwa wafanyakazi wa ofisi za usalama kama vile jeshi na polisi kwa kuwashtaki kuwa wapelelezi nchini Uganda.

Msemaji wa Polisi nchini Uganda, Emilian Kayima ametangazia BBC kuwa anayekamatwa yeyote huwa ana uhalifu anaotuhumiwa.

“ Walikamtwa kutoka pande zote za nchi, sijui idadi yao lakini huwa wanatuhumiwa uhalifu mbalimbali” Emilian amesema

“ Raia wengine kama Waganda hukamatwa wanapotuhumiwa uhalifu fulani, serikali ya Rwanda pia inajua kuwa hatutesi Wanyarwanda” ameongeza

Kayima amehakikisha wengi mwa hawa  Wanyarwanda  wanaokamatwa  huwa hawana vitambulisho rasmi,na Waganda huwa wanajihuisha na ujambazi.

Pamoja na hayo, Wanyarwanda karibu 1000 walikamatwa na kufungiwa nchini Uganda,Baadhi yao walitangazia vyombo vya habari kuwa walikuenda nchini Uganda kutafuta ajira.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com