Home HABARI Serikali ya Uganda inakwenda kuwafukuza raia wa Burundi zaidi elfu 40
HABARI - February 16, 2017

Serikali ya Uganda inakwenda kuwafukuza raia wa Burundi zaidi elfu 40

Serikali ya Uganda inasema ya kwamba wanakwenda kuelekeza wakimbizi elfu 46 wa Burundi katika nchi yao ambao walikuwa ukimbizini.

Uganda inahakikisha ya kuwa Burundi kuna amani na kwa hayo hakuna sababu ya kubaki ukimbizini.

Maamzi hayo nia baada ya uhamasishaji wa serikali ya Burundi huko Uganda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakiwaomba kurudi kwao.

Hillary Onek anayehusika na wakimbizi Uganda, amesema ya kuwa Warundi ambao watakataa kurudi kwao watapewa vitambulisho vya miezi tatu vya kuishi Uganda.

Eti “munakwenda kupewa Visa ya kuishi hapa miezi tatu, na muda ukikwisha hatutawafukuza kama Trump ila tutawaomba kurudi katika nchi yenu kwa haraka”.

Hata kama huyu waziri anasema hao, mwakilishi wake katika wizara, Musa Ecweru yeye ni kinyume na hayo kwa kuwa yeye anasema ya kuwa hakuna mkimbizi ataye fukuzwa Uganda isipo kuwa kwa mapenzi yake mwenyewe kama vile hutangaza Deutch Welle. Na hayo ni sheria kimataifa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanao husika na haki za wakimbizi katika bara la Afrika wanasema ya kuwa viongozi hao hawaambatane kwa misemi inaonekana ya kuwa hawajui yanayo fanyika Burundi.

Tangu mwaka wa 2015 warundi wengi wamekimbia nchi yao kwa sababu ya mizozo ilio zuka wakati Rais Nkurunziza aliamua kuwania mhura wa tatu.

Hadi sasa maongezi ya pande ambazo kubishana yanaendelea Tanzania, ila maamzi yanakosekana kwa sababu wanasema mpatanishi wao yupo na upendeleo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.